Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DR Congo yaipiga kidude Benin huko Morocco

DR CONGO Pict

Muktasari:

  • Bao la kipindi cha kwanza la kiungo Theo Bongonda lilitosha kuipa DR Congo ya kocha Sebastien Desabre ushindi wao muhimu katika mechi ya kwanza ya mashindano ya Afcon 2025 mbele ya Benin mchezo uliofanyika uwanjani Al Barid.

RABAT, MOROCCO: UKUTA wa Aaron Wan-Bissaka, Chancel Mbemba, Axel Tuanzebe na Arthur Masuaku ulikuwa kizingiti kikubwa kwa washambuliaji wa Benin kupenya na hivyo kusababisha timu yao kuchapwa bao 1-0 na DR Congo kwenye mchezo wao wa kwanza wa Kundi D katika mashindano ya Afcon 2025 yanayozidi kunoga huko Morocco.

Bao la kipindi cha kwanza la kiungo Theo Bongonda lilitosha kuipa DR Congo ya kocha Sebastien Desabre ushindi wao muhimu katika mechi ya kwanza ya mashindano ya Afcon 2025 mbele ya Benin mchezo uliofanyika uwanjani Al Barid.

Katika mchezo huo, Benin ilianza na straika Tosin Aiyegun, anayekipiga kwenye kikosi cha Lorient ya Ufaransa, lakini hakuonekana kabisa kuwa na maajabu mbele ya ukuta imara DR Congo, ambao ulioundwa na mastaa kadhaa wenye uzoefu wa kucheza kwenye Ligi Kuu England na hivyo kumfanya kocha Desabre aandikishe ushindi wa kwanza kwenye Afcon 2025 ya huko Morocco bila ya presha yoyote. Bongonda alifunga bao hilo pekee baada ya kazi nzuri ya ya Masuaku.

DR 02

Kocha, Desabre aliamua kuanza na mshambuliaji Cedric Bakambu, anayekipiga Real Betis kabla ya kuja kumtoa kwenye dakika tano za mwisho na kumwingiza straika wa zamani wa Yanga, anayekipiga Pyramids FC, Fiston Mayele.

Katika mchezo huo, DR Congo iliiacha Benin kuwa na umiliki wa mpira kwa muda mwingi, ikifanya hivyo kwa asilimia 61 huku wao wakimiliki mpira kwa asilimia 39, ambazo walitumia kupiga mashuti saba, matatu yakilenga goli na manne yakipita mbali, huku Benin yenyewe ilipiga mashuti tisa, huu mawili tu ndiyo yaliyolenga goli.

Hata hivyo, ukuta wa DR Congo ulifanya kazi ya ziada kutokana na kuzuia mashuti matatu ya Benin, wakati wao walishuhudia shuti lao moja tu ndiyo lililozuiwa katika mechi hiyo, ambayo ilishuhudia kona 10 zikipigwa, tano kwa kila upande.

DR 01

DR Congo ilipiga krosi 14 dhidi ya 21 za Benin, huku kikosi cha Desabre kikifanya madhambi mara 16 dhidi ya 11 ya Benin inayonolewa na Gernot Rohr, wakati chama la kina Mayele lilifanya mashambulizi ya kushtukiza mara sita, wakati Benin ilifanya hivyo mara mbili tu. Makipa wote, Lionel Nzau Mpasi wa DR Congo na Saturnin Allagbe wa Benin walifanya sevu mbili kila mmoja, katika mechi iliyokuwa imejaa mashambulizi ya kupeanza zamu.