Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dikembe Mutombo afariki dunia

Muktasari:

  • Rambirambi nyingi zimetumwa kwa gwiji huyo, ambaye alichaguliwa mara nane tofauti kwenye kikosi cha All-Star na alihesabika kama mmoja wa walinzi bora kabisa kuwahi kutokea kwenye mchezo huo wa kikapu.

LOS ANGELES, MAREKANI: SUPASTAA wa zamani wa NBA, Dikembe Mutombo amefariki dunia akiwa umri wa miaka 58.
Mkali huyo wa mpira wa kikapu aliyewahi kuchaguliwa kwenye Hall of Fame, akiwa na kimo cha futi 7 na inchi 2, amefariki dunia kwa saratani ya ubongo.

Mutombo alitumikia miaka 18 akicheza kwenye NBA katika timu bora kabisa.

Rambirambi nyingi zimetumwa kwa gwiji huyo, ambaye alichaguliwa mara nane tofauti kwenye kikosi cha All-Star na alihesabika kama mmoja wa walinzi bora kabisa kuwahi kutokea kwenye mchezo huo wa kikapu.

Taarifa kutoka kwa kamishina wa NBA, Adam Silver ilibainisha: “Dikembe Mutombo alikuwa mkubwa kuliko maisha. Ndani ya uwanja alikuwa mzuiaji bora na beki bora kwenye historia ya NBA.

Nje ya uwanja alikuwa na moyo wa kipekee kabisa wa kusaidia wengine. Hakuna mtu aliyefanikiwa kumzidi Dikembe katika shughuli za kuwa balozi wa dunia wa NBA. Alikuwa na moyo wa kiutu. Alipenda mpira wa kikaku hivyo alifanya kila aliloweza kulieneza hilo kwenye jamii, hasa huko kwao Jamhuri ya Kidemokrasia Congo na barani kote Afrika.

“Nilipata nafasi ya kusafiri na Dikembe sehemu nyingi za dunia na kuona kile ambacho amefanya katika kuwainua watu. Muda wote alikuwa akipatikana kwenye matukio ya mwaka ya NBA, akiwa na tabasamu pana, sauti ya kishindo na ile staili yake ya kupepea kidole iliyotambulisha kwenye rika zote za mashabiki.”

Mutombo alianza maisha yake ya mchezo wa kikapu mwaka 1991 akiwa na timu ya Denver Nuggets. Baada ya hapo alikwenda kuzichezea Atlanta Hawks, Philadelphia 76ers, New Jersey Nets na New York Knicks. Alistaafu akiwa na Houston Rockets mwaka 2009.

Licha ya kwamba hajawahi kushinda ubingwa, Mutombo alichaguliwa mara nane tofauti kwenye timu ya All-Star. Alichaguliwa kuwa Mlinzi Bora wa Mwaka mara nne tofauti. Baada ya kustaafu, Mutombo alijishughulisha na kazi za kibinadamu.