Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Delap atibua hesabu Chelsea

DELAP Pict

Muktasari:

  • Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca alithibitisha majeraha ya mchezaji huyo yatamfanya kuwa nje hadi Desemba mwaka huu.

LONDON, ENGLAND: STRAIKA Liam Delap atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 10 hadi 12 baada ya kupatwa na maumivu ya misuli ya paja.

Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca alithibitisha majeraha ya mchezaji huyo yatamfanya kuwa nje hadi Desemba mwaka huu.

Delap, 22, alipata majeraha hayo kwenye mechi ya ushindi wa mabao 2-0 iliyopata Chelsea dhidi ya Fulham mwishoni mwa mwezi uliopita.

Alitolewa na kuingizwa Tyrique George dakika 14 ya mchezo baada ya kupatiwa matibabu ndani ya uwanja jana kushindwa kuendelea na mechi.

Majeraha yake yalitishia kuvuruga uhamisho wa Nicolas Jackson kwenda Bayern Munich, kabla ya kuamua kumrudisha Marc Guiu kikosini kuja kuongeza nguvu kwenye fowadi hiyo ya miamba ya Stamford Bridge.

Delap ndiyo kwanza amejiunga na Chelsea, Juni mwaka huu akitokea kwenye kikosi cha Ipswich Town kwa ada ya Pauni 30 milioni.

Sasa mchezaji mwenzake mpya, Joao Pedro atawajibika kuongoza safu ya ushambuliaji ya miamba hiyo ya Stamford Bridge.

Mbrazili huyo, Pedro amekuwa na mwanzo mzuri huko Stamford Bridge baada ya kusajiliwa akitokea Brighton kwa ada ya Pauni 60 milioni. Tayari ameshafunga mabao mawili na kuasisti mara mbili katika mechi tatu alizochezea The Blues kwenye Ligi Kuu England msimu huu.