Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dani Olmo pasua kichwa Barca

Muktasari:

  • Olmo alijiunga na Barcelona akitokea RB Leipzig kwa ada ya Pauni 50 milioni kwenye dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, lakini hali ngumu ya kiuchumi ya klabu hiyo iliwafanya wamwandikishe mchezaji huyo kwa hati ya muda hadi mwishoni mwa 2024.

BARCELONA, HISPANIA: BARCELONA ipo kwenye hatari ya kumpoteza Dani Olmo baada ya kukwama kwenye rufaa ya kumwandikisha mchezaji huyo kwenye kikosi.

Olmo alijiunga na Barcelona akitokea RB Leipzig kwa ada ya Pauni 50 milioni kwenye dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, lakini hali ngumu ya kiuchumi ya klabu hiyo iliwafanya wamwandikishe mchezaji huyo kwa hati ya muda hadi mwishoni mwa 2024.

Na Barca ilikuwa inapambana kuhakikisha inamwandikisha Olmo aendelee kutumikia ambapo mwisho wa kufanya hivyo ilikuwa jana, Desemba 31.

Kutokana na hilo, Barca ilipeleka jambo hilo mahakamani ili kujaribu kumwandikisha kwenye La Liga mchezaji huyo, lakini wameshindwa kesi.

Kwa mujibu wa Marca, hata rufaa waliyokata nayo imetupwa kando. Na sasa Barca inatafuta njia mbadala ya kuhakikisha inamwandikisha Olmo na kuwa kwenye kikosi - la watampoteza bure kabisa kwenye dirisha la uhamisho wa Januari lililofunguliwa leo, Jumatano.

Olmo aliweka kipengele kwenye mkataba wake kinachomruhusu kuondoka Nou Camp bure kabisa kama timu hiyo itakwama kwa namna yoyote kumwandikisha kuitumikia timu hiyo kutokana na sababu za kifedha. Hivyo, Olmo atakuwa na ruhusa ya kuanza mazungumzo na klabu nyingine kama Barca itashindwa kabisa.

Suluhisho moja lililobaki kwa Barca ni kuuza eneo moja la kukaa watu maarufu kwenye uwanja wao wa Camp Nou kwa wawekezaji wa Mashariki ya Kati kwa miaka 20 kwa dau linalodaiwa kuwa ni Pauni 82.9 milioni. Hilo likifanyika, Barca itaweza kukidhi viwango vya kifedha na hivyo kuwa na uwezo wa kumwaandikisha Olmo na mchezaji mwenzake Pau Victor kwenye kikosi. Olmo kuna timu kibao zinamtaka ikiwamo Manchester City, Manchester United na Arsenal.