Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Daka ana bahati hajavunja shingo

Muktasari:

  • Straika huyo, Daka, 27, alifunga bao hilo dakika za majeruhi katika mechi hiyo ya hatua ya makundi ya Afcon 2025 na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mali.

CASABLANCA, MOROCCO: STAA wa Leicester City, Patson Daka amenusurika kuvunjika shingo wakati alipojaribu kuruka sarakasi na kuangukia shingo wakati alipokuwa akishangilia bao aliloifungia Zambia bao la kusawazisha kwenye mashindano ya Afcon 2025.

Straika huyo, Daka, 27, alifunga bao hilo dakika za majeruhi katika mechi hiyo ya hatua ya makundi ya Afcon 2025 na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mali.

Daka alifunga kwa kichwa cha kuchumpa kusawazisha bao la Mali lililofungwa na Lassine Sinayoko. Katika mechi hiyo, Mali ilipoteza nafasi ya ushindi, kufuatia El Bilal Toure kumkosa mkwaju wa penalti kwenye kipindi cha kwanza.

Lakini, Daka staili yake ya kushangilia baada ya kufunga nusura imweke kwenye matatizo makubwa, ikiwamo kuvunjika shingo mikono kuteleza wakati anajaribu kubinuka sarakasi uwanjani Stade Mohammed V mjini Casablanca.

Shabiki wa kwanza alisema: “Kaka alijaribu kuonyesha sarakasi yake na kujikuta kwenye maumivu ya shingo, natumaini haikuwa siriazi sana!”

Mwingine aliongeza: “Daka alijaribu kuruka sarakasi. Shangilia kawaida kaka, maumivu ya shingo sio ya mchezo.”

Shabiki wa tatu alisema: “Hii ndio ile mtu akikuuliza ilikuwaje 2025.”

Na shabiki wa nne alisema: “Afcon sasa imeanza rasmi. Huu ushangiliaji bora Afcon. Uwe poa, Patson!”

Staa huyo alijiunga na Leicester City kwa ada ya Pauni 23 milioni akitokea RB Salzburg mwaka 2021.