Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cristiano Ronaldo ‘amkataa’ dada yake

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Dada yake mkubwa, Katia Aveiro, alinukuliwa nchini Ureno akisema kuwa nahodha huyo wa Ureno angehitimisha safari yake ya kimataifa baada ya mashindano haya.

TORONTO, CANADA: MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo amekanusha madai yaliyotolewa na dada yake kwamba ana mpango wa kustaafu kuchezea timu ya taifa mara baada ya Kombe la Dunia kumalizika.

Dada yake mkubwa, Katia Aveiro, alinukuliwa nchini Ureno akisema kuwa nahodha huyo wa Ureno angehitimisha safari yake ya kimataifa baada ya mashindano haya.

Kauli hiyo ilitolewa dakika chache kabla ya mchezo wa hatua ya 32 bora kati ya Ureno na Croatia uliochezwa leo Ijumaa asubuhi mjini Toronto.

RONA 01

Katika mchezo huo, Ronaldo mwenye umri wa miaka 41 alifunga bao muhimu la penalti dakika ya 68 na kusawazisha matokeo kuwa 1-1.

Kikosi cha kocha Roberto Martinez baadaye kilipata ushindi katika dakika za majeruhi kupitia bao la Goncalo Ramos.

Baada ya mechi, Ronaldo alizungumzia mustakabali wake na kusema:

“Mustakabali wangu si jambo muhimu kwa sasa. Nitakuwa na muda baadaye, baada ya kushinda au kupoteza, kuzungumza na familia yangu kisha nitafanya uamuzi bora.

RONA 02

“Sifanyi tena uamuzi kwa papara. Sasa kila kitu kinafanywa kwa utulivu. Kilicho muhimu ni kufurahia wakati uliopo”€

Kabla ya mechi, Katia Aveiro alinukuliwa akisema:“Kwa taarifa nilizonazo kutoka kwa chanzo cha kuaminika, naamini huu ndiyo utakuwa mchezo wake wa mwisho, hivyo tufurahie.

Naamini si leo atakapoaga, lakini muda huo unakaribia. Ninaamini kwa dhati huu ndio mwisho wake. Hivyo furahieni sana, kwa sababu itakuwa vigumu kumpata mwingine atakayefunga mabao 200. Ninazungumzia timu ya taifa ya Ureno.

RONA 03

Mshambuliaji huyo wa Al-Nassr FC alifunga bao lake la tatu katika Kombe hili la Dunia, lililofanyika nchini Canada, na kuisaidia Ureno kusonga mbele.

Hili ni Kombe la Dunia la sita kwa Ronaldo, akiendelea kuongeza rekodi nyingi alizoweka katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili akiwa na timu ya taifa.

Katika hatua ya makundi, alifunga mabao mawili dhidi ya Uzbekistan na kusherehekea kwa kupaza sauti, “NIMERUDI!” mbele ya kamera.

Bao dhidi ya Croatia lilikuwa la kwanza kwa Ronaldo katika hatua za mtoano za Kombe la Dunia baada ya mechi 10 mfululizo bila kufunga katika hatua hiyo.

Mapema katika mchezo huo, alikaribia kufunga baada ya kutuliza pasi nzuri na kumalizia kwa ustadi akiwa karibu na lango, lakini bao hilo lilikataliwa kutokana na kuotea.

Ronaldo, ambaye msimu uliopita alitwaa taji lake la kwanza akiwa Saudi Arabia, sasa ameichezea Ureno mechi 232, rekodi ya taifa hilo, na kufunga mabao 146, ambayo pia ni rekodi.

Kwa upande wa klabu, alifunga mabao 30 katika mechi 35 za Al-Nassr msimu uliopita, na tangu ajiunge na klabu hiyo amefunga mabao 123 katika mechi 142. Sasa Ureno inajiandaa kuvaana na Hispania katika mchezo wa hatua ya 16 bora utakaochezwa Jumatatu mjini Dallas.