Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cristiano Ronaldo akerwa na kelele “Messi, Messi” Saudia

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Al Nassr waliifunga Al-Shabab mabao 4-2 katika mchezo huo muhimu wa Saudi Pro League uliokuwa na presha kubwa kwenye mbio za ubingwa, ambapo chama hilo la Ronaldo lilijihakikishia pointi zilizoliweka juu ya msimamo kwa pointi 82 dhidi ya Al Hilal yenye 77.

RIYADH, SAUDI ARABIA: SUPASTAA wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo (CR7) alipata wakati mgumu kukabiliana na mashabiki walioanza kuimba jina la Lionel Messi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Saudi Arabia dhidi ya Al-Shabab, jana.

Katika mechi hiyo ambayo Ronaldo aliendelea kusogea karibu zaidi na rekodi ya mabao 1,000, mashabiki kutoka jukwaani walisikika wakipiga kelele “Messi, Messi” wakimkejeli nyota huyo wa Ureno kutokana na kiwango chake cha kawaida katika mechi za hivi karibuni.

Awali, Ronaldo hakukasirika wala kuonyesha dalili za kuathiriwa na kelele hizo, badala yake, aliinua mikono yake kana kwamba anaongoza bendi akionyesha kuwa hajali kejeli kutoka kwa mashabiki, lakini baadaye alibadilika na kuanza kuonyesha kukasirishwa.

RONAL 01

Al Nassr waliifunga Al-Shabab mabao 4-2 katika mchezo huo muhimu wa Saudi Pro League uliokuwa na presha kubwa kwenye mbio za ubingwa, ambapo chama hilo la Ronaldo lilijihakikishia pointi zilizoliweka juu ya msimamo kwa pointi 82 dhidi ya Al Hilal yenye 77.

Kwa bao lake katika mchezo huo, nyota huyo sasa amefikisha mabao 971 katika maisha yake ya soka, akibakiwa na 29  kufikia rekodi ya kihistoria ya mabao 1,000, jambo ambalo halijawahi kufikiwa na mchezaji yeyote katika soka la kulipwa. Hata hivyo, nyota wa mchezo alikuwa Joao Felix.

Mshambuliaji huyo wa Ureno alifunga hat trick ya kuvutia, ambapo alianza kufunga dakika ya tatu kabla ya kuongeza bao la pili dakika ya 10.

RONAL 02

Baadaye Yannick Carrasco aliifungia Al-Shabab bao dakika ya 30. Ronaldo aliandika jina lake kwenye orodha ya wafungaji kipindi cha pili baada ya kufunga dakika ya 75, bao lililowafanya mashabiki wa Al Nassr kushangilia kwa nguvu. Felix alikamilisha hat trick yake dakika ya 98 kwa mkwaju wa penalti.