Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CHUPUCHUPU :Van Persie aigomea Chelsea Old Trafford

Didier Drogba

Muktasari:

Man United ilitumia nafasi hiyo kupiga mpira wa adhabu, uliopigwa na Di Maria na kuunganishwa kwa kichwa na Marouane Fellaini kabla ya kipa kuupangua na Van Persie kumalizia kwa shuti kali lililoifanya timu hiyo ya Louis van Gaal kutoka uwanjani na pointi moja.

NGOMA ya wanaume. Straika Robin van Persie alifunga kwenye dakika za majeruhi kuigomea Chelsea kuondoka na pointi zote tatu Old Trafford wakati Manchester United ilipoambulia sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika jana Jumapili.

Man United ikiwa nyumbani iliduwazwa kwenye dakika 53 baada ya straika Didier Drogba kufunga kwa kichwa kufuatia kona ya Cesc Fabregas na kuonekana kama kikosi hicho cha Jose Mourinho kingeondoka uwanjani hapo na ushindi.

Mchezo huo ulishuhudia United ikipoteza nafasi kadhaa za kufunga kupitia kwa Van Persie na Chelsea ikipoteza nafasi yake ya kufunga kufipitia kwa Eden Hazard.

Baada ya kupata bao hilo la kuongoza, Mourinho alionekana kujihami baada ya kuongeza viungo wa kukaba wakati alipomtoa Oscar na kumwingiza Obi Mikel, huku wenyeji wakizidi kufanya mashambulizi yao kwa kupitia pembeni kushoto alikokuwa Angel Di Maria na kulia alikocheza Adnan Januzaj.

Kwenye mchezo huo, Chelsea ilishuhudia wachezaji wake saba wakionyeshwa kadi za njano huku beki wake Branislav Ivanovic kuonyeshwa nyekundu baada ya kuonyesha kadi mbili za njano kwenye dakika za majeruhi baada ya kumchezea rafu Di Maria na kusababisha faulo nje ya eneo la hatari la Chelsea.

Man United ilitumia nafasi hiyo kupiga mpira wa adhabu, uliopigwa na Di Maria na kuunganishwa kwa kichwa na Marouane Fellaini kabla ya kipa kuupangua na Van Persie kumalizia kwa shuti kali lililoifanya timu hiyo ya Louis van Gaal kutoka uwanjani na pointi moja.

Kwa matokeo hayo, United imefikisha pointi 13 na kuendelea kubaki kwenye nafasi ya nane, wakati Chelsea imezidi kujikita kileleni baada ya kufikia pointi 23.

Matokeo mengine ya ligi hiyo, straika Samuel Eto’o alifunga mara mbili kuisaidia Everton kuichapa Burnley 3-1 ugenini. Bao jingine la kikosi hicho cha Goodinson Park liliwekwa kimiani na Romelu Lukaku, wakati Burnley ilipata bao lake kupitia kwa Danny Ings.

Kwingineko, Tottenham Hotspur ikiwa nyumbani White Hart Lane ilikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Newcastle United.

Straika Emmanuel Adebayor alifunga bao la kuongoza kwa Spurs katika dakika ya 18, lakini Newcastle ilirudi kwa kasi kubwa kwenye kipindi cha pili na Sammy Ameobi akitokea benchi alitumia sekunde sita tu kufunga bao la kusawazisha kwenye dakika ya 46 kabla ya Ayoze kupiga la pili la ushindi kwa kikosi cha Newcastle chenye maskani yake St James’ Park.