Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chido Obi: Kinda anayefunga sana anatua UTD

Muktasari:

  • Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 16 ni mmoja wa mastaa waliotajwa kuwa na vipaji vikubwa kabisa kwenye kikosi cha Arsenal.

MANCHESTER, ENGLAND: HABARI ndo hiyo. Manchester United imefanikiwa kunasa huduma ya kinda Chido Obi-Martin kutoka Arsenal, imeelezwa.

Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 16 ni mmoja wa mastaa waliotajwa kuwa na vipaji vikubwa kabisa kwenye kikosi cha Arsenal.

Obi-Martin alihusishwa na uhamisho wa kutua Man United huko nyuma na sasa imethibitishwa atakwenda kukipiga Old Trafford kwa mujibu wa Fabrizio Romano.

Gwiji huyo wa masuala ya usajili na uhamisho, Fabrizio aliposti kwenye Twitter, alipoandika: “Chido Obi Martin anakwenda Man United. Straika huyo mwenye kipaji kikubwa ataachana na Arsenal na amekubali ofa ya Man United.

“Huo ni mwelekeo wa Chido ambaye amekataa ofa kubwa zaidi kutoka Ujerumani ili tu ajiunge na Man United. Mipango ya Man United imemshawishi mshambuliaji huyo mzaliwa wa mwaka 2007 kukubali kutua Old Trafford.”

Arsenal ilimpa ofa mchezaji huyo kupata namba kwenye kikosi cha U18 na atacheza pia kwenye U21 na atafanya mazoezi na kikosi cha kwanza. Lakini, fowadi huyo anayefunga sana, alitaka nafasi ya moja kwa moja kwenye kikosi cha U21.

Obi-Martin alifunga mabao 29 katika mechi 17 za ligi alizochezea Arsenal kwenye kikosi cha U18 msimu uliopita.

Februari mwaka huu alikuwa gumzo baada ya kufunga mabao 10 katika mechi moja, wakati Arsenal ya vijana chini ya miaka 16 ilipocheza na Liverpool. Suala la kufunga kwa kinda huyo halijawahi kuwa shida na alifunga mara nne katika kila mechi dhidi ya Crystal Palace na Fulham.

Alifunga mabao matano dhidi ya West Ham na mabao saba katika mechi moja dhidi ya Norwich City. Alijiunga na Arsenal mwaka 2022 akitokea kwenye timu ya KB ya Denmark. Obi-Martin ameiwakilisha Denmark kwenye Euro 2024 kwa timu za vijana chini ya miaka 17 na katika mechi za makundi, alifunga mabao mawili katika mechi tatu.