Chelsea yaacha vifaa Kombe la Dunia

Muktasari:
- Kwenye orodha hiyo ya mastaa waliotemwa kikosini ni pamoja na wakali Raheem Sterling na Joao Felix. Kwenye fainali hizo, Chelsea inayonolewa na kocha Enzo Maresca imepangwa kwenye kundi moja pamoja na LAFC ya Marekani, Flamengo ya Brazil na Esperance ya Tunisia.
LOS ANGELES, MAREKANI: CHELSEA imepiga chini mastaa wenye thamani ya Pauni 150 milioni katika kikosi chake kitakachokwenda kuchuana kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu litakalofanyika Marekani mwezi huu.
Kwenye orodha hiyo ya mastaa waliotemwa kikosini ni pamoja na wakali Raheem Sterling na Joao Felix. Kwenye fainali hizo, Chelsea inayonolewa na kocha Enzo Maresca imepangwa kwenye kundi moja pamoja na LAFC ya Marekani, Flamengo ya Brazil na Esperance ya Tunisia.
Katika kuelekea fainali hizo, kocha wa The Blues amefanya uamuzi mgumu kwenye kikosi chake.
Sterling mwenye thamani ya Pauni 50 milioni ameachwa baada ya kuwa na wakati mbaya alipokuwa kwa mkopo Arsenal, wakati Felix aliyenaswa kwa Pauni 45 milioni naye amewekwa kando kwa kiwango chake.
Felix alikuwa kwa mkopo AC Milan. Beki Axel Disasi ni miongoni mwa wachezaji ambao waliwekwa kando kwenye kikosi baada ya kutumikia nusu ya msimu uliopita kwa mkopo huko Aston Villa.
Lakini, kitu kilichoshangaza wengi ni kutemwa kwa kipa Djordje Petrovic. Mserbia huyo alitarajiwa kuwamo kwenye kikosi baada ya Chelsea kushindwa kukamilisha dili la kumnasa kipa wa Ufaransa, Mike Maignan kutoka AC Milan.
Petrovic alisema kwa kiwango bora kwa mkopo Strasbourg msimu uliopita na alitazamiwa kuja kuongeza ushindani wa namba golinii, lakini kocha Maresca ameamua kwanda na Robert Sánchez, Filip Jorgensen na Mike Penders kwenye fainali hizo.