Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick atia neno afya ya Fergie

Muktasari:

  • Carrick ambaye aliwahi kucheza chini ya Ferguson kwa mafanikio makubwa, alisema alipata taarifa hizo kabla ya  mchezo wa mchezo huo wa Ligi Kuu England na zikamuathiri moja kwa moja kisaikolojia.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa muda wa Manchester United, Michael Carrick ameweka wazi jinsi alivyoguswa na taarifa za ghafla kuhusu afya ya Sir Alex Ferguson, aliyekimbizwa hospitali muda mfupi kabla ya mechi dhidi ya Liverpool.

Carrick ambaye aliwahi kucheza chini ya Ferguson kwa mafanikio makubwa, alisema alipata taarifa hizo kabla ya  mchezo wa mchezo huo wa Ligi Kuu England na zikamuathiri moja kwa moja kisaikolojia.

“Nilisikia taarifa kabla ya mechi na ukweli ni kwamba iliniathiri sana. Tunatumaini yuko salama na anapata nafuu haraka,” alisema Carrick.

Awali, hali ya sintofahamu ilitanda katika dimba la Old Trafford baada ya Ferguson (84) kuripotiwa kujisikia vibaya akiwa uwanjani huku akifanya kile alichozoea kuhudhuria mechi za timu yake ya zamani.

Taarifa zinaeleza kuwa alipewa huduma ya kwanza ndani ya uwanja kabla ya kupelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi.

Hata hivyo, vyanzo vya karibu vimeeleza kuwa hali yake kwa sasa “iko sawa” baada ya kupata matibabu, jambo lililowatuliza mashabiki wengi.

Licha ya presha hiyo nje ya uwanja, Manchester United iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Liverpool. Carrick anaamini ushindi huo unaweza kuwa faraja kwa Ferguson wakati akiendelea kupata nafuu.

Ferguson, ambaye pia aliwahi kuinoa Aberdeen FC kabla ya kutengeneza historia kubwa Old Trafford, anaendelea kuheshimiwa kama mmoja wa makocha bora kabisa kuwahi kutokea huku afya yake ikiwa jambo linalofuatiliwa kwa karibu na wengi.

Ferguson alijijengea heshima kubwa akiwa kocha wa Manchester United kwa miaka 26, akiiwezesha klabu hiyo kuwa moja ya timu zenye mafanikio makubwa duniani. Katika kipindi hicho, aliiongoza United kushinda mataji 13 ya Ligi Kuu England, matano ya FA Cup na manne ya League Cup, huku akikusanya jumla ya makombe 38.

Katika michuano ya Ulaya, Ferguson aliitwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1999 na 2008, ikumbukwe kuwa aliweka historia  ya kubeba “Treble” mwaka 1999 (Ligi, FA Cup na Ligi ya Mabingwa Ulaya).