Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carragher ataka beki tatu Liverpool

Muktasari:

  • Bado haielewi kama Liverpool itafanya usajili dirisha la Januari baada ya kikosi hicho cha Kocha Arne Slot kufanya vizuri msimu huu ikiongoza msimamo wa Ligi Kuu England na ule wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

LIVERPOOL, ENGLAND: BEKI wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher amewaambia mabosi wa timu hiyo kuhakikisha wanafanya usajili wa beki wa kushoto dirisha la Januari ili kuja kumsaidia Andy Robertson, ambaye kwa sasa anapambana na hali yake.

Bado haielewi kama Liverpool itafanya usajili dirisha la Januari baada ya kikosi hicho cha Kocha Arne Slot kufanya vizuri msimu huu ikiongoza msimamo wa Ligi Kuu England na ule wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwenye usajili, eneo ambalo wanapaswa kulizingatia ni beki ya kushoto na Robertson, 30, anaonekana kushuka kiwango. Nahodha huyo wa Scotland alionyeshwa kadi nyekundu dakika 17 katika mchezo wa wikiendi iliyopita wakati Liverpool ilipopata sare ya 2-2 dhidi ya Fulham uwanjani Anfield.

Kutokana na hilo, Carragher anaamini kocha Slot ataleta mchezaji mwingine kwenye nafasi hiyo ya beki wa kushoto wakati dirisha la Januari litakapofunguliwa.

“Robertson anakabiliwa na wakati mgumu kwenye nafasi yake,” alisema Carragher.

“Dhidi ya Fulham alionekana kuwa na shida kabla ya kuonyeshwa kadi nyekundu. Anahitaji msaada. Liverpool haina mbadala wake kitu ambacho wanapaswa kukipatia suluhu kwenye dirisha la Januari.”

Beki wa Bournemouth, Milos Kerkez, ambaye amekuwa na msimu mzuri ni mmoja wa wachezaji wanaodaiwa kupigiwa hesabu za Liverpool pamoja na klabu nyingine kubwa kwenye Ligi Kuu England.

Carragher anaamini Kerkez ataweza kuja kumpa changamoto ya namba Robertson na saini yake inaweza kuwa nyepesi kwa kupitia kwa mkurugenzi wa michezo mpya wa Liverpool, Richard Hughes, ambaye ndiye aliyefanikiwa usajili wa beki huyo huko Bournemouth.

“Kerkez anafanya vizuri Bournemouth. Mkurugenzi wa ufundi aliyemsajili Bournemouth (Richard Hughes) kwa sasa ni mkurugenzi wa michezo Liverpool,” alisema Carragher, ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka baada ya kustaafu mchezo huo.