Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bruno Fernandes apigiwa debe mchezaji bora EPL

BRUNO Pict

Muktasari:

  • Fernandes ni miongoni mwa wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo baada ya kuwa na msimu bora.

MANCHESTER, ENGLAND: MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Benjamin Sesko amempigia debe nahodha wake, Bruno Fernandes kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu wa Ligi Kuu England 2025/26 huku akisifu mchango wake.

Fernandes ni miongoni mwa wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo baada ya kuwa na msimu bora.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 tayari ana pasi za mabao 18 msimu huu, akikaribia rekodi ya juu zaidi tangu mwaka 1992.

Katika msimu wake wa kwanza England, Sesko amefunga mabao tisa kwenye ligi na manne kati ya hayo yalitokana na pasi za Fernandes. 

BRU 01

Sesko amesema anajifunza mambo mengi kutoka kwake: “Ninapata maelekezo mengi sana kutoka kwa Bruno mazoezini na wakati mwingine kabla ya mazoezi. Kitu chochote anachokuambia, huwa anapenda ukifanye bila kusita. Nashukuru sana kupata nafasi ya kuwa karibu naye.”

Alipoulizwa kama anaamini Fernandes anapaswa kushinda tuzo hiyo, Sesko alijibu: “Ni mchezaji mkubwa. Ni mwenzangu na lazima nisimame upande wake. Ndiyo, anastahili kushinda.”

BRU 02

Manchester United leo usiku, Jumatatu ilitupa karata yake muhimu katika hekaheka za ligi hiyo dhidi ya Brentford, kusaka pointi sita ili kujikatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kwa upande wake, kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick, amesema mafanikio ya Fernandes yanatokana na uhuru anaopata uwanjani.

Tangu Carrick arejee, Fernandes amehusika katika mabao mengi zaidi, amefunga matatu na kutoa pasi tisa za mabao.