Brazil yaichapa Scotland, Neymar arudisha mzuka
Muktasari:
- Mabao mawili ya mshambuliaji Vinicius Junior dakika ya Saba akitumia asisti na Rayan na lile la pili dakika ya 45+3 akitengenezewa na Bruno Guimares yakatosha kuipeleka Brazil mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao 2-0.
Brazil imefanikiwa kumaliza kinara wa kundi lake ikikata tiketi ya kutinga hatua ya 32 bora, ikiichapa Scotland kwa mabao 3-0, ikimaliza kibabe mechi za makundi.
Mabao mawili ya mshambuliaji Vinicius Junior dakika ya Saba akitumia asisti na Rayan na lile la pili dakika ya 45+3 akitengenezewa na Bruno Guimares yakatosha kuipeleka Brazil mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao 2-0.
Vinicius alikaribia kupiga bao la tatu dakika ya 22 lakini VAR ikalikataa baada ya kubainika, kabla ya kufunga bao hilo alimchezea madhambi mchezaji wa Scotland.
Mabao hayo mawili yanamfanya Vinicius kuwa kinara wa ufungaji kwenye mechi za makundi kwenye kundi hilo akifikisha jumla ya mabao manne, akifunga kwenye mechi zote tatu.
Kipindi cha pili Brazil ikaendelea kutafuta ushindi mkubwa zaidi ikitengeneza mashambulizi mengi lakini ikakosa umakini wa kuyatumia.
Mshambuliaji Matheus Cunha akaipatia bao la mwisho Brazil kwenye mchezo huo dakika ya 60 akimalizia asisti ya Guimares, likiwa ni bao lake la tatu kwenye mechi tatu za makundi.
Mshambuliaji Neymar Jr hatimaye akafanikiwa kurudi uwanjani akicheza kwa mara ya kwanza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026 akiiingia dakika ya 76 akichukua nafasi ya Cunha.
Wakati Neymar akiingia uwanjani mashabiki maelfu wa Brazil wameshangilia kwa nguvu kuona staa huyo anarudi Uwanjani akafanikiwa kupiga shuti moja pekee lililolenga lango ambapo mara baada ya mchezo huo kumalizika, akajikuta anatokwanna machozi kwa hatua ya kurejea kwake uwanjani .
Mpaka kukamilika kwa dakika 90 za mchezo huo Brazil ikafanikiwa kuondoka na ushindi huo wa mabao 3-0, ikienda kuongoza kundi lake C ikifisha jumla ya pointi saba.
Chini ya Brazil ipo Morocco iliyomaliza na pointi kama hizo lakini ikizidiwa tofauti ya mabao ya kufungwa na kufungwa na vinara hao, huku Scotland ikimaliza nafasi ya tatu na na pointi tatu wakati Haiti ikishika mkia bila pointi yoyote.