Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bissouma kuikosa mechi ya ufunguzi AFCON 2025

MBESUMA Pict

Muktasari:

  • Mechi ya leo inatrajiwa kuwakutanisha wachezaji waliowahi kucheza pamoja Yanga na kutwaa mataji ya Ligi Kuu, Kombe la FA na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, kipa Djigui Diarra aliyepo Mali na straika wa Zambia, Kennedy Musonda.

MALI itamkosa kiungo nyota anayekipiga Tottenham Hotspur, Yves Bissouma katika mechi ya ufunguzi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) itakayochezwa leo Jumatatu, lakini kocha wa timu hiyo, Tom Saintfiet ana imani nyota huyo atakuwa na mchango chanya katika michuanop hiyo ya 35 inayofanyika Morocco.

Bissouma ni mmoja wa wachezaji watatu ambao hawatakuwepo katika mechi ya Kundi A dhidi ya Zambia itakayochezwa Casablanca. Wengine ni beki wa kati Sikou Niakate na beki wa kulia Hamari Traoré.

Bissouma, mwenye umri wa miaka 29, bado hajacheza hata mechi moja kwa Spurs tangu alipoondolewa kikosini kabla ya pambano la Super Cup dhidi ya Paris Saint-Germain Agosti mwaka huu.

Baadaye alifanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu baada ya kuumia akiwa anacheza mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Dakika 72 alizocheza dhidi ya Madagascar ndizo pekee amepata msimu huu hadi sasa.

Saintfiet amesema jana umapili kuwa, Bissouma tayari anaendelea na mazoezi na anaweza kuzingatiwa kucheza katika mechi ya pili ya makundi dhidi ya wenyeji Morocco, itakayochezwa Rabat siku ya Ijumaa.

MBESU 01

“Katika mashindano mengi makubwa, kuna wachezaji huanza wakiwa na majeraha lakini baadaye huwa hatari zaidi katika robo fainali, nusu fainali au hata fainali,” amesema kocha huyo wa Mali na kuongeza;

“Yves ni nahodha wangu, ni mchezaji muhimu, ni kiongozi wa timu yetu, na tuna uhakika kwamba Yves atakuwa tayari wakati wa mashindano. Kadri mechi zinavyozidi kuwa ngumu, tutafurahi kuwa naye pamoja nasi. Tunamhitaji nahodha ambaye yupo tayari kiakili na kimwili.”

Mechi ya leo inatrajiwa kuwakutanisha wachezaji waliowahi kucheza pamoja Yanga na kutwaa mataji ya Ligi Kuu, Kombe la FA na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, kipa Djigui Diarra aliyepo Mali na straika wa Zambia, Kennedy Musonda.