Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bilionea amtikisa Florentino Perez Real Madrid

BILIONEA Pict

Muktasari:

  • Rais huyo ameiongoza Madrid kwa jumla ya miaka 23 tangu mwaka 2000 na aliwahi  kujiuzulu mwaka 2006 kabla ya kurejea tena mwaka 2009.

MADRID, HISPANIA: BILIONEA mmoja mkubwa anaripotiwa kuwa tayari kumpa changamoto rais wa muda mrefu wa Real Madrid, Florentino Perez, katika uchaguzi wa urais wa klabu hiyo.

Katika mkutano wa waandishi wa habari uliotikisa uliofanyika Jumanne mchana, Perez ambaye ni rais wa sasa wa Madrid alithibitisha kuwa ameiomba bodi ya klabu kupanga uchaguzi mpya, licha ya kuchaguliwa tena bila kupingwa Januari 2025.

“Nimeiomba Bodi kuanzisha mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, ambapo bodi ya sasa pia itashiriki,  kama kuna mtu anayetaka kugombea, huu ndio wakati wake.” amesema Perez.

Rais huyo ameiongoza Madrid kwa jumla ya miaka 23 tangu mwaka 2000 na aliwahi  kujiuzulu mwaka 2006 kabla ya kurejea tena mwaka 2009.

Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 79, hajawahi kupata mpinzani rasmi tangu aanze muhula wake wa pili, jambo ambalo limechangiwa na uwepo wa watu wachache sana wanaoweza kupata fedha zinazohitajika kwa ajili ya kugombea nafasi hiyo.

BILI 01

Hata hivyo, safari hii mambo yanaweza kubadilika kwani mfanyabiashara kutoka Jiji la Alicante, Enrique Riquelme, ambaye ni rais wa kampuni ya maji na nishati ya Grupo Cox, anaripotiwa kuwa tayari kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho kwa mujibu wa gazeti la MARCA.

Kwa upande mwingine, chombo kingine cha habari cha Hispania, El Confidencial, kimeripoti kuwa Riquelme tayari ameshakusanya kiwango cha fedha kinachohitajika ili kuingia rasmi katika mbio za kuwania urais wa klabu hiyo.

Riquelme pia anadaiwa kuhudhuria hafla iliyowakutanisha wanachama wa klabu hiyo Aprili mwaka huu, ingawa taarifa zaidi kuhusu hafla hiyo hazijawekwa wazi.

Tofauti na klabu nyingine nyingi, mgombea urais wa Real Madrid lazima atimize masharti makali yaliyoainishwa katika katiba ya klabu hiyo ili kuruhusiwa kushiriki uchaguzi.

Moja ya masharti hayo ni kuhakikisha ana dhamana ya kifedha inayofikia karibu asilimia 15 ya bajeti ya sasa ya klabu. Kwa mujibu wa tovuti ya AS, kiwango hicho kwa sasa ni takribani Euro milioni 189 (zaidi ya shilingi 575 bilioni).

BILI 02

Pia lazima kuwepo dhamana ya benki inayokubalika kisheria chini ya sheria za Hispania pamoja na taratibu za klabu.

Benki husika pia inapaswa kuthibitisha kuwa dhamana hiyo inatokana na mali binafsi za wagombea wenyewe.

Mbali na hilo, mgombea lazima awe mwanachama wa Real Madrid kwa kipindi kisichopungua miaka 20 kabla ya kugombea.

Pia mgombea haruhusiwi kuwa anafanya kazi yoyote katika klabu nyingine ya soka wakati wa kuwasilisha maombi yake ya kugombea.