Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Besidei yamtia hatiani Lamine Yamal

YAMAL Pict

Muktasari:

  • Mkali huyo wa Barcelona na Hispania alitumia wikiendi iliyopita kufanya sherehe ya kutimiza miaka 18 na ilihudhuriwa na mastaa kibao wenye majina makubwa, lakini sasa mambo yametibuka.

BARCELONA, HISPANIA: KINDA wa Barcelona, Lamine Yamal ameripotiwa kufanyiwa uchunguzi na mamlaka za usalama baada ya kuripotiwa kuajiri mbilikimo kutumbuza kwenye sherehe yake ya kutimiza miaka 18.

Mkali huyo wa Barcelona na Hispania alitumia wikiendi iliyopita kufanya sherehe ya kutimiza miaka 18 na ilihudhuriwa na mastaa kibao wenye majina makubwa, lakini sasa mambo yametibuka.

Video zimekuwa zikizagaa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha mbilikimo kadhaa wakiondoka kutoka kwenye sherehe hiyo ya Yamal.

Jambo hilo limeibua maofisa wa serikali kuanza kufanya uchunguzi kama kweli mbilikimo walitumika kuburudisha kwenye sherehe hiyo.

Hilo limedaiwa kuwaibua viongozi wa chama watu wenye tatizo hilo hilo Hispania, ADEE na kufikiria kumchukua hatua za kisheria kinda huyo.

Rais wa ADEE, Carolina Puente alisema: “Haikubaliki kwenye karne hii ya 21, watu wenye tatizo la kutokuwa na kimo kirefu kutumika kuburudisha kwenye sherehe za watu binafsi. Na kinachoshangaza zaidi ni kwamba mtu huyo anayehusika ni maarufu Lamine Yamal.”

Mamlaka za serikali za Hispania zinaonekana kuguswa na jambo hilo na kuanzisha uchunguzi wa kuona kama kweli jambo hilo lilifanyika kwa mbilikimo kuburudisha wageni wapatao 200 waliohudhuria kwenye shereke ya kuzaliwa Yamal. Endapo kama Yamal atakutwa na hatia, basi anaweza kukabiliwa na adhabu ya kulipa faini Pauni 867,000.