Benzema ahukumiwa kifungo mwaka mmoja

Wednesday November 24 2021
benzema pic

PARIS, UFARANSA. STAA wa Real Madrid, Karim  Benzema amekutwa na hatia ya kujipatia kipato kwa njia zisizo sahihi kwa kumtishia mchezaji mwenzake  Mathieu Valbuena kwamba angetoa video zake za faragha ikiwa asingempatia pesa.
Benzema amehukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja  sambamba na kupingwa faini ya Pauni 63,000 (sawa na Sh193 milioni za kitanzani) katika hukumu iliyotolewa na mahakama iliyopo huko  Versailles, karibu kabisa na Jiji la Paris .
Mawakili kwa upande wa serikali walisema Benzema alikuwa akifanya kazi na moja ya kundi la wahuni huko nchini Ufaransa na ndio alikuwa akitumika kumshawishi Valbuena, 37, atoe pesa ili video zisivujishwe.
Mbali ya Benzema mwenyewe, marafiki zake wa zamani wanne pia walikutwa kwenye hatia hiyo ya kumlazimisha Valbuena kutoa pesa ili wasivunjishe video.
Upande wa mawakili waBenzema umesisitiza kwamba haujakubaliana na uamuzi huo na wamepanga kukata rufaa ili kesi isikilizwe  tena kwani mteja wao hana hatia.

Advertisement