Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bellingham hata yeye haelewi

Muktasari:

  • Madrid imeshinda mechi moja tu kati ya tano za hivi karibuni kwenye LaLiga, jambo linalomweka Alonso kwenye hatari ya kufukuzwa kazi baada ya miezi michache tu tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Bayer Leverkusen.

MADRID,HISPANIA: STAA wa Real Madrid, Jude Bellingham benchi la ufundi la timu hiyo bado linapambana kujua kwanini hawapati matokeo chanya katika mechi za hivi karibuni lakini wao kama wachezaji wanamuunga mkono kocha Xabi Alonso, licha ya kuwapo kwa presha kubwa kutoka kwa mashabiki wanaotaka afukuzwe.

Madrid imeshinda mechi moja tu kati ya tano za hivi karibuni kwenye LaLiga, jambo linalomweka Alonso kwenye hatari ya kufukuzwa kazi baada ya miezi michache tu tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Bayer Leverkusen.

Bellingham, ambaye alikosa nafasi nzuri ya kuisawazisha Real Madrid dhidi ya Manchester City, alikiri kuwa hata yeye  anashindwa kuelewa ni kwa nini timu yake imeshuka kiwango.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa  England, mwenye umri wa miaka 22, akizungumza na  TNT Sports alisema: “Bado sisi kama wachezaji tunajaribu kutafakari juu ya kile kinachoendelea. Kuna nyakati ambapo naona tunapaswa kustahimili lakini tunashindwa na mwisho tunapoteza. Nina imani msimu bado haujaisha licha ya kwamba tupo katika kipindi kibaya.”

Bellingham pia alithibitisha kuwa yeye na wenzake wanaamini Alonso hapaswi kufukuzwa kwa sababu ni miongoni mwa makocha bora na wanapendezwa na mbinu zake.

“Kwa asilimia mia, kocha amekuwa bora. Tulikuwa na kikao kwenye timu na tuliamini tungeondokana na hali hii, lakini haijawa kama tulivyotarajia. Bado tunapambana na kuendelea kupigana,” alisema kiungo huyo Nuingereza.