Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Chelsea ala shavu Kombe la Dunia dakika za jionii

Muktasari:

  • Nyota huyo amepata nafasi hiyo baada ya beki wa Newcastle United, Tino Livramento kuondolewa katika kikosi hicho dakika za mwisho baada ya kupata majeraha ya misuli, ikiwa ni siku moja imebaki kabla ya England kucheza mechi yake na Croatia.

TEXAS, MAREKANI: BEKI wa kulia wa Klabu ya Chelsea, Trevoh Chalobah amechaguliwa dakika za jioni kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya England, kinachojianda kuanza kampeni ya Kombe la Dunia kwa mechi yake ya kwanza ya kundi L kesho dhidi ya Croatia.

Nyota huyo amepata nafasi hiyo baada ya beki wa Newcastle United, Tino Livramento kuondolewa katika kikosi hicho dakika za mwisho baada ya kupata majeraha ya misuli, ikiwa ni siku moja imebaki kabla ya England kucheza mechi yake na Croatia.

Livramento mwenye miaka 23, amepata majeraha hayo ambayo hatoweza kushiriki tena michuano hiyo ya Kombe la Dunia, jambo lililompa nafasi Kocha Mkuu wa England, Thomas Tuchel kumjumuisha Trevoh Chalobah katika kikosi hicho cha 'Three Lions'. 

Timu zinazoshiriki Michuano ya Kombe la Dunia zinaruhusiwa kufanya mabadiliko kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 26 hadi saa 24, kabla ya mechi yao ya kwanza ya hatua ya makundi, japo ikitokea mchezaji atakuwa amepata majeraha hayo.

Chama cha Soka cha England (FA), kilisema mchezaji huyo alipata majeraha wakati akiwa mazoezi siku ya Jumapili ya Juni 14, 2026.

"Vipimo na tathmini ya kitabibu iliyofanyika Jumatatu kwa bahati mbaya vilithibitisha Livramento hatashiriki tena katika mashindano haya kwa England, tunasikitika kwa ajili yako, Tino na tunakutakia nafuu ya haraka," ilieleza taarifa hiyo.

Livramento, ambaye tayari ameichezea England mara sita, ameshiriki karibu kila mechi ya timu hiyo mwaka 2026, isipokuwa ushindi wa kirafiki wa timu hiyo wa mabao 3-0, dhidi ya Costa Rica, Juni 11, 2026, ambao ndio pekee hakuweza kucheza.

Beki huyo alikuwa miongoni mwa mabeki wenye uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali ambao waliteuliwa na kocha Thomas Tuchel kwa ajili ya mashindano haya, huku Livramento akicheza pia beki wa kushoto kuanzia England na Klabu ya Newcastle United. 

Wachezaji wengine kama Dan Burn, Djed Spence na Jarell Quansah pia wamekuwa wakitumika katika nafasi tofauti kwa klabu zao na timu ya taifa.

Kwa upande wa Trevoh Chalobah, mwenye miaka 26, ameichezea England mara moja tu, Juni 2025 dhidi ya Senegal katika mechi ambayo England ilipoteza kwa kuchapwa mabao 3-1, ikiwa ni mechi ya pili ya Kocha, Tuchel tangu ateuliwe kikosini humo.

Licha ya Chalobah kujumuishwa kwenye kikosi cha England kwa mechi za kufuzu dhidi ya Serbia na Albania zilizopigwa mwaka jana, ila beki huyo hakupata nafasi ya kucheza, japo kwa sasa amepata fursa hiyo tena baada ya kuumia kwa Livramento.

Chalobah alipata nafasi yake ya kwanza ya kung'ara Chelsea chini ya Tuchel mwaka 2021, ambapo Katika kipindi cha miezi 12, chini ya kocha huyo, alicheza mechi 31 na kufunga mabao manne na sasa amemjumuisha tena kwenye kikosi cha England.

Tangu mechi ya mwisho ya Chelsea Mei 24, 2026, Chalobah ameendelea kuwa katika kiwango kizuri cha utimamu wa mwili akiwa ni mshindi wa Kombe la Dunia la Klabu la mwaka 2025, huku kwa msimu wa 2025-2026, akiichezea Chelsea jumla ya mechi 47.