Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Borussia awazia kipute cha Madrid

Muktasari:

  • Dortmund imekuwa na mwenendo mzuri kwenye fainali hizo hadi sasa, lakini kwenda kukabiliana na Real Madrid kumeanza kuwapa presha kwa sababu wanafahamu wazi Los Blancos ndiyo wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda.

MIAMI, MAREKANI: WAKATI Real Madrid ikijiandaa sasa kwa mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia la Klabu, beki wa Borussia Dortmund, ambao watakuwa wapinzani wao kwenye hatua hiyo, Yan Couto amekiri kwamba siku hiyo patachimbika.

Dortmund imekuwa na mwenendo mzuri kwenye fainali hizo hadi sasa, lakini kwenda kukabiliana na Real Madrid kumeanza kuwapa presha kwa sababu wanafahamu wazi Los Blancos ndiyo wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda.

“Tumekuwa na michuano mizuri na kiwango chetu kimekuwa kikiongeza baada ya kila mechi,” alisema Couto na kuongeza. “Lakini, hii itakwenda kuwa mechi ngumu sana dhidi ya Madrid. Yatupasa kupambana na kuwa na ndoto kama tunataka kupata kitu kikubwa.

“Tuna kila kitu cha kutufanya tuwe na kiwango bora kwenye mechi dhidi ya Madrid.”

Real Madrid, inayoongozwa na kocha Xabi Alonso, imeonekana kuwa tishio kwenye michuano hiyo huku uzoefu na mastaa wake kuwapa nafasi ya kufanya vizuri zaidi.

Dortmund itahitaji kupambana kwelikweli kuidhibiti Real Madrid, hasa mastaa wao Gonzalo Garcia na Jude Bellingham ambao wamekuwa na njaa zaidi ya mabao.

Beki Couto alimsifu pia kocha Alonso akisema: “Xabi ni kocha mahiri. Anastahili sifa kwa kile alichokifanya kwa miaka miwili Leverkusen. Kwenye mwaka mmoja alishinda kila kitu na mwaka uliofuatia alishika namba mbili. Huu ni mwanzo tu wa kazi yake.”