Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Arsenal adai kuna presha ya ubingwa

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta kitakaa pamoja wiki hii kujadili kwa kina jinsi wanavyopaswa kucheza pale mechi zinapokuwa na presha kubwa. Arsenal iliifunga Chelsea mabao 2-1, Jumapili na kuongeza pengo lao kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England kufikia pointi tano.

LONDON, ENGLAND: BEKI wa boli, Jurrien Timber amekiri kuwa wachezaji wa Arsenal wanaweza kuhisi hali ya wasiwasi ndani ya Uwanja wa Emirates wakati mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England zikiingia kwenye hatua muhimu.

Kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta kitakaa pamoja wiki hii kujadili kwa kina jinsi wanavyopaswa kucheza pale mechi zinapokuwa na presha kubwa. Arsenal iliifunga Chelsea mabao 2-1, Jumapili na kuongeza pengo lao kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England kufikia pointi tano.

Lakini, hata baada ya Chelsea kubaki na wachezaji 10 kwa dakika 20 za mwisho, mchezo uliisha kwa presha kubwa na Timber aliweza kuhisi wasiwasi kutoka kwa mashabiki uwanjani.

Beki huyo wa Arsenal alisema: “Bila shaka unahisi, hasa mwishoni. Tulipunguza kasi ya kucheza kidogo, jambo ambalo halikuwa la lazima hasa ukiwa na mchezaji mmoja zaidi. Ni jambo tunalopaswa kulifanyia kazi na kulizungumzia pia, kwa sababu tayari limetokea mara kadhaa msimu huu. Na hasa kwa sababu unaweka nguvu nyingi kwenye mchezo, unacheza vizuri sana hasa kipindi cha kwanza na ulipaswa kuwa mbele 1-0 au 2-0 mapema. Lakini mambo kama haya hutokea hasa dhidi ya timu nzuri kama Chelsea kwa hiyo ni jambo ambalo lazima tulijadili.

“Imetokea pia msimu huu kwamba tuliweza kustahimili presha ilipoongezeka, lakini pia mara kadhaa hatukuweza. Ni sehemu ya mchezo na unapaswa kuelewa kinachotokea wakati huo, nishati iliyopo uwanjani na kwa mashabiki, wasiwasi ninaouzungumzia. Ni jambo unalopaswa kulikabili na kulizungumzia, lakini tunapaswa kulidhibiti vizuri.”

Arsenal, ambayo itasafiri kwenda kucheza na Brighton, Jumatano, sasa imebakiwa na mechi tisa tu za ligi. Malengo yao ni kushinda taji la Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza baada ya miaka 22, ikitaka kufanya hivyo kufuatia kumaliza nafasi ya pili kwa misimu mitatu mfululizo.

Timber ni mmoja wa wachezaji saba pekee katika kikosi cha Arsenal waliowahi kushinda ubingwa wa ligi, baada ya kuisaidia Ajax kushinda taji la Ligi Kuu Uholanzi mara mbili.

Hata hivyo, beki huyo ameeleza kuwa hali hiyo haiwezi kulinganishwa na ushindani mkali dhidi ya Manchester City katika Ligi Kuu England. Man City iko nyuma kwa pointi tano dhidi ya Arsenal, lakini miamba hiyo ya Etihad inayonolewa na Pep Guardiola ina mchezo mmoja mkononi.