Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo Arsenal wakomaa na Sesko, Gyokeres

TETESI Pict

Muktasari:

  • Mabosi wa Arsenal wanahitaji kusajili straika kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ushambuliaji ambalo limekuwa na mapungufu tangu kuanza kwa msimu huu.

ARSENAL kwa sasa imewekeza nguvu zote katika mazungumzo na wawakilishi wa straika wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Slovenia, Benjamin Sesko, 21, pamoja na straika wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya Sweden, Viktor Gyokeres kumsajili mmoja wao dirisha la majira ya kiangazi.

Mabosi wa Arsenal wanahitaji kusajili straika kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ushambuliaji ambalo limekuwa na mapungufu tangu kuanza kwa msimu huu.

Hata hivyo, mchakato wa kupata huduma ya mmoja kati ya mastaa hawa unaonekana kuwa mgumu kwa asilimia kubwa kutokana na wingi wa timu ambazo zinawahitaji.

Kila straika kati ya hawa wawili anagharimu zaidi ya Pauni 70 milioni kiasi ambacho Arsenal huenda ikapata tabu kukitoa kwani tayari inadaiwa kufikia makubaliano ya kusajili wachezaji wa maeneo mengine, hivyo pesa itakayobakia inaweza ikawaangusha kwenye vita ya kuwawania mafundi hawa ikiwa wapinzani wao wataweka mpunga wa maana.


Jamie Gittens

NEWCASTLE United imeanza mazungumzo ya kumsajili winga wa  Borussia Dortmund na timu ya taifa ya vijana ya England, Jamie Gittens dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Mbali ya Gittens, Newcastle pia inahitaji saini ya kipa wa Dortmund,  Gregor Kobel, 27.


Jamie Vardy

STRAIKA wa Leicester City, Jamie Vardy ambaye ametangaza ataachana na timu hiyo mwisho wa msimu huu, inadaiwa kawaambia wawakilishi wake bado anataka kuendelea kucheza Ligi Kuu England kwa msimu mmoja zaidi ikiaminika unaweza kuwa msimu wake wa mwisho kabla ya kutundika daruga. Vardy mwenye umri wa miaka 38, alitangaza kuondoka Leicester mwishoni mwa msimu huu.


Dayot Upamecano

MAZUNGUMZO kati ya wawakilishi wa Bayern Munich na beki wao wa kimataifa wa Ufaransa, Dayot Upamecano, 26, yameshaanza yakiwa na lengo la kufanikisha mchakato wa staa huyo kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia hadi mwaka 2030. Upamecano ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Bayern na msimu huu alihusika kwa kiasi kikubwa kuisaidia timu hiyo kushinda taji la Bundesliga.


Nuno Tavares

LAZIO inataka kuilipa Arsenal Pauni 7.5 milioni dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ajili ya kumnunua mazima beki wa kushoto wa  timu hiyo ambaye ni raia wa Ureno, Nuno Tavares.

Mabosi wa Lazio wanataka kutoa kiasi hicho cha pesa baada ya ripoti ya kocha wao kusisitiza asajiliwe kwani ameridhishwa na kiwango alichoonyesha msimu huu na anacheza kwa mkopo.


Rasmus Hojlund

STRAIKA wa Manchester United na timu ya taifa ya Denmark,  Rasmus Hojlund, 22, yupo njiapanda juu ya hatma yake akiwa hajapewa taarifa yoyote ikiwa kocha wa timu hiyo Ruben Amorim angependa kuendelea kuwa naye kwa msimu ujao au la. Rasmus ambaye huduma yake inahitajika na timu lukuki kutoka Italia, kiwango alichoonyesha tangu Amorim apewe mikoba hakionekani kumshawishi kocha huyo.


Milos Kerkez

BOURNEMOUTH inataka kiasi kisichopungua Pauni 45 milioni kutoka kwa timu yoyote inayohitaji saini ya beki wao wa kushoto, Milos Kerkez ambaye anawindwa ma vigogo mbalimbali barani ulaya dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Staa huyu mwenye umri wa miaka 21, anapewa nafasi kubwa ya kujiunga na Liverpool.


Sven Botman

BEKI kisiki wa Newcastle, Sven Botman anataka kuendelea kusalia katika kikosi hicho licha ya kupata ofa kutoka Paris St-Germain inayohitaji kumsajili mara baada ya msimu huu kumalizika.

Staa huyu wa kimataifa wa Uholanzi kwa sasa ana umri wa miaka 25, na amekuwa mmoja kati ya mastaa tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Newcastle tangu kuanza kwa msimu huu.