Barcelona mbona kazi wanayo

BARCELONA, HISPANIA. BAADHI ya wachezaji wapya wa Barcelona huenda wakaukosa mechi ya La Liga kesho, dhidi ya Rayo Vallecano kwani bado hawajawaandikisha bodi ya ligi hiyo.
Wakati miamba hiyo ikiendelea na mchakato wa kupata suluhisho, huenda Frankie de Jong na Memphis Depay wakapigwa bei kutokana na kanuni ya La Liga.
Awali Barcelona ilitegemea mchakato wa kuandikisha wachezaji wao wapya (Robert Lewandowski, Raphinha, Frankie Kessie, Andreas Christensen, Jules Kounde) utakamalika kabla ya mechi ya kwanza ya La Liga itakayoanza kesho. Aidha kwa upande wa Ousmane Dembele ameongeza mkataba wa miaka miwili lakini hatacheza hadi atakapoandikishwa bodi ya ligi.
Wiki ikiyopita Rais wa Barcelona, Joan Laporta aliwaondoa hofu mashabiki kuhusu mchakato huo kwani wapo katika hatua nzuri.
“Hakuna tatizo wachezaji watatambulishwa, tupo katika hatua nzuri na wachezaji wapya watapata stahiki wanazostahili,” alisema Laporta.