Barca hoi, Bayern, Inter zapeta UEFA

LONDON, ENGLAND. MIAMBA ya soka Hispania, Barcelona imepokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Inter Milan, kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikijiweka katika hatari ya kutosonga mbele hatua inayofuata ya michuano inayofuata huku Xavi akichukizwa na maamuzi mabovu ya refa.
Inter Milan ilipata bao pekee la ushindi kupitia nyota wao Hakan Çalhanoğlu dakika ya 45 tuya mtananange huo.
Licha ya ushindi wa Inter Milan imeendelea kushika nafasi ya pili kwenye kundi lao C ikiwa na pointi 6, Barcelona ikishika nafasi ya tatu yenye pointi 3 huku vinara wa kundi Bayern Munich wao wana pointi tisa baada ya kuichapa Viktoria Plzen mabao 5-0 uwanja wa Allianz Arena.
Matokeo mengine ya mechi za Ligi Mabingwa Ulaya, Liverpool iliibuka na ushindi wa mabo 2-0 dhidi ya Rangers,vijana wa Jurgrn Klopp walihitaji ushindi kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele baada ya kushinda michezo miwili.
Matokeo mengine Ajax ilipokea kichapo cha mabao 6-1 ilipomenyana na Napoli, Atletico Madrid ikifungwa mabao 2-0 dhidi ya Club Brugge, Tottenham ikatoka suluhu dhidi ya Eintracht Frankfurt, Marseille ikaibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Sporting Lisbon, FC Porto ikiiadhibu Bayer Leverkuson mabao 2-0.