Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Austria yaigomea Algeria zikifuzu hatua ya mtoano

AUSTRIA Pict

Muktasari:

  • Austria ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 28 likifungwa na mshambuliaji, Marko Arnautovic akimalizia pasi ndefu ya beki, David Alaba.

Algeria na Austria zimefanikiwa kufuzu hatua ya mtoano baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi uliokuwa na ushindani mkali.

Austria ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 28 likifungwa na mshambuliaji, Marko Arnautovic akimalizia pasi ndefu ya beki, David Alaba.

Algeria ilikaribia kusawazisha bao hilo dakika ya 36 lakini shuti la Ibrahim Maza likagonga mwamba na kurudi uwanjani.

Dakika ya 45, Algeria ikafanikiwa kusawazisha bao hilo likifungwa na beki, Rafik Belghali, aliyewatoka mabeki wa Austria na kuachia shuti kali, timu hizo zikaenda mapumziko kwa sare ya bao 1-1.

AUST 01

Kipindi cha pili, kiungo Marcel Sabitzer alifanikiwa kuirudisha Austria kwenye uongozi akifunga bao kwa shuti kali, akipokea pasi safi kutoka kulia ya Konrad Laimer.

Algeria ikafanikiwa kusawazisha tena dakika ya 60 kwa bao la shuti kali kutoka kwa winga na nahodha wake, Riyad Mahrez akipokea pasi nzuri ya Houssem Aouar kutoka upande wa kushoto.

Mahrez tena akafunga bao la tatu ambalo kwake lilikuwa la pili dakika ya 90+3 akitengenezewa na yuleyule Aouar akiitanguliza Algeria kwa mara ya kwanza kwenye mchezo huo.

AUST 02

Wakati Algeria ikiona kama imeshinda, Austria ikasawazisha dakika ya 90+6 kupitia mshambuliaji Sasa Kalajdzic ambaye aliingia uwanjani dakika moja iliyopita, akipokea pasi ya Michael Gregoritsch na kuifanya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya mabao 3-3.

Matokeo hayo yanalifanya kundi J kuongozwa na Argentina iliyomaliza na pointi tisa, ikifuatiwa na Austria na Algeria kila moja ikiwa na pointi nne, wakati Jordan haina kitu.

Algeria sasa itakwenda kukutana na Uswizi kwenye mchezo wa mtoano huku Austria ikikutana na Hispania, wakati Argentina ikiikabili Cape Verde.