Aubrey Modiba anautaka ubingwa CAFCL
Muktasari:
- Modiba, ambaye ndiye aliyefunga bao pekee la ushindi (1-0) katika mchezo wa kwanza nchini Afrika Kusini, amekiri kuwa mtihani uliopo mbele yao ni mgumu lakini unawezekana.
Beki na kiungo wa Mamelodi Sundowns, Aubrey Modiba, amewataka wachezaji wenzake kubaki na mtazamo chanya kuelekea mchezo wa mkondo wa pili wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), dhidi ya AS FAR mwishoni mwa wiki hii huko Rabat, Morocco.
Modiba, ambaye ndiye aliyefunga bao pekee la ushindi (1-0) katika mchezo wa kwanza nchini Afrika Kusini, amekiri kuwa mtihani uliopo mbele yao ni mgumu lakini unawezekana.
“Tunapaswa kujipanga na kufikiria mambo mazuri kuelekea mechi yetu inayofuata. Ninaamini tumeanza vizuri nyumbani, kwa hakika tutapambana ugenini na kupata matokeo yatakayotupa ubingwa wa Afrika msimu huu,” amesema Modiba.
Mamelodi Sundowns inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ugenini ili kutangazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Afrika msimu huu.
Mechi hii ya mkondo wa pili wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) itachezwa Jumapili, Mei 24, 2026 kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah uliopo mjini Rabat, Morocco saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania.