Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aubameyang kukosa moja AFCON 2025

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Gabon imepangwa kuvaana na Cameroon, Jumatano ijayo na Auba mwenye umri wa miaka 36, ambaye kwa muda mrefu amekuwa nguzo muhimu ya timu ya taifa ya Gabon, alipata jeraha katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) Jumapili iliyopita, wakati klabu ya Olympique de Marseille ilipoifunga AS Monaco.

MSHAMBULIAJI mkongwe Pierre-Emerick Aubameyang ataukosa mchezo wa kwanza wa Gabon katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) litakaloanza wikiendi hii lakini anatarajiwa kupona jeraha la paja na kuweza kucheza mechi mbili zinazofuata za Kundi F katika fainali hizo za Morocco.

Gabon imepangwa kuvaana na Cameroon, Jumatano ijayo na Auba mwenye umri wa miaka 36, ambaye kwa muda mrefu amekuwa nguzo muhimu ya timu ya taifa ya Gabon, alipata jeraha katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) Jumapili iliyopita, wakati klabu ya Olympique de Marseille ilipoifunga AS Monaco.

Kutokana na hali hiyo, Shirikisho la Soka la Gabon lilisema, nyota huyo ataendelea kubaki Ufaransa kwa ajili ya matibabu kabla ya kujiunga na kikosi cha taifa.

“Timu ya madaktari wa Olympique de Marseille iliomba Aubameyang apatiwe matibabu akiwa Marseille baada ya kushauriana na madaktari wa timu ya taifa,” ilisema taarifa ya shirikisho hilo.

“Taarifa za kitabibu zinaonyesha kuwa mchezaji hatakuwa tayari kucheza mechi ya Desemba 24 dhidi ya Cameroon. Hata hivyo, kulingana na maendeleo ya afya yake na matokeo ya vipimo vya kitabibu, kuna uwezekano wa kushiriki mechi itayofuata Desemba 28 dhidi ya Msumbiji.” Mechi zote mbili zitapigwa mjini Agadir.

Gabon, itacheza dhidi ya watetezi wa taji, Ivory Coast Desemba 31 huko Marrakech, pia huenda wakalazimika kufanya mabadiliko katika safu ya ulinzi, baada ya beki wa kati wa Metz, Michel Mboula kuwa na shaka ya kushiriki mashindano hayo kutokana na jeraha la paja