Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aston Villa yamtosa jumla Rashford

Muktasari:

  • Fowadi huyo Mwingereza alitumikia nusu ya pili ya msimu uliopita kwa mkopo huko Villa Park baada ya kutibuana na kocha Ruben Amorim huko Old Trafford.

BIRMINGHAM, ENGLAND: ASTON Villa imethibitisha kwamba hatamsajili jumla winga wa Manchester United, Marcus Rashford.

Fowadi huyo Mwingereza alitumikia nusu ya pili ya msimu uliopita kwa mkopo huko Villa Park baada ya kutibuana na kocha Ruben Amorim huko Old Trafford.

Aston Villa inayonolewa na Unai Emery ilikuw ana makubaliano ya kulipa Pauni 40 milioni ili kumchukua jumla Rashford baada ya msimu kumalizika. Rashford, 27, alicheza vizuri huko Villa Park, ambako alifunga mabao manne na kuasisti mara sita katika mechi 17 kabla ya kupata majeraha katika kuelekea siku za mwisho za msimu.

Iliripotiwa huko nyuma kwamba Aston Villa ilikuwa na mpango wa kutomsajili staa huyo, lakini haikuwa imethibitisha hilo hadi sasa ilipotoa taarifa rasmi. Aston Villa ilibainisha Rashford atarudi Old Trafford, wakati wachezaji wenzake waliokuwa kwa mkopo pia Marco Asensio na Axel Disasi nao wamerudi kwenye timu zao Paris Saint-Germain na Chelsea mtawalia.

Taarifa ya Aston Villa ilisomeka: “Marco Asensio, Marcus Rashford na Axel Disasi waliojiunga Aston Villa, Februari kwa mkopo hadi mwisho wa msimu wa 2024/25. Kiungo mshambuliaji Asensio alisema mechi 21, alifunga mabao manane, ikiwamo matau kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya Club Brugge.

“Forward Rashford alicheza mechi 17  ja kuchangia mabao tisa katika michuano yote, akifunga mara mbili kwenye robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Preston North End.

“Beki Disasi aliwasili kutoka Chelsea na kucheza mechi 10 hapa Aston Villa, mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Ipswich Town katikati Februari. Kila mtu Aston Villa angewatakia kila la heri wachezaji hao kwa jitihada zao kwenye klabu, hivyo tunawaombea heri kwenye maisha yao.â€

Wakati huo huo, Aston Villa imethibitisha wachezaji Robin Olsen na Kourtney Hause wameondoka kwenye klabu hiyo baada ya mikataba yao kufika ukingoni. Uamuzi huo wa Aston Villa sasa unamwaacha Rashford kwenye sintofahamu kubwa ya mustakabali wa soka lake.