Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta kicheko Havertz yupo fiti

Muktasari:

  • Fowadi huyo Mjerumani alitazamiwa kuwa nje ya uwanja hadi mwisho wa msimu baada ya kusumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja tangu Januari, lakini sasa atarejea uwanjani kwa haraka.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema supastaa wake Kai Havertz anakaribia kurudi uwanjani kabla ya msimu kumalizika na hilo linaongeza mzuka zaidi kwenye kikosi hicho kabla ya mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain.

Fowadi huyo Mjerumani alitazamiwa kuwa nje ya uwanja hadi mwisho wa msimu baada ya kusumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja tangu Januari, lakini sasa atarejea uwanjani kwa haraka.

Arteta alisema Havertz atarejea uwanjani baadaye mwezi huu, wakati Arsenal ikiwa na ndoto kubwa za kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kocha huyo Mhispaniola alisema: "Nahisi itakuwa hivyo. Kama kila kitu kitakwenda vizuri, mpango uliopo atacheza kwenye mechi chache zilizobaki msimu huu."

Kocha Arteta alifichua pia kiungo Jorginho naye ana nafasi kubwa ya kurudi uwanjani baada ya kuwa nje kwa wiki kadhaa. Arsenal ilitarajia kukipiga na Bournemouth usiku wa Jumamosi, ambapo ushindi kwenye mechi hiyo utakuwa umewahakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye hatua ya nusu fainali dhidi ya PSG itapigwa Jumatano ijayo, huku miamba hiyo ya Emirates ikienda Parc des Princes ikiwa nyuma kwa bao 1-0, walilofungwa na Ousmane Dembele wiki iliyopita.

"Kitu pekee tunachoweza kukifanya ni kiwango chetu na hisia zetu. Lakini, tuna vitu kadhaa bado tunavitaka kwenye Ligi Kuu England," alisema Arteta.