Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sare yaipeleka Japan 32 Bora Kombe la Dunia, kukutana na Brazil

Muktasari:

  • Mechi hiyo ya leo ya kundi F, iliyopigwa kwenye Uwanja wa Dallas ulipo mji wa Arlington, jimbo la Texas, Marekani, licha ya Japan kutawala mchezo huo, ila ilishindwa kutumia faida hiyo na hadi dakika 45, za kipindi cha kwanza timu hizo zikaenda suluhu ya (0-0).

SARE ya bao 1-1, iliyoipata Japan dhidi ya Sweden leo imeihakikishia kufuzu hatua ya 32 bora, ya Kombe la Dunia, baada ya kumaliza nafasi ya pili katika kundi F, ikiwa na pointi tano na sasa itakutana na Brazil iliyomaliza vinara wa kundi C na ponti saba, katika mechi itakayopigwa Jumatatu ya Juni 29, 2026.

Mechi hiyo ya leo ya kundi F, iliyopigwa kwenye Uwanja wa Dallas ulipo mji wa Arlington, jimbo la Texas, Marekani, licha ya Japan kutawala mchezo huo, ila ilishindwa kutumia faida hiyo na hadi dakika 45, za kipindi cha kwanza timu hizo zikaenda suluhu ya (0-0).

Kipindi cha pili, Japan iliendelea na kasi yake ya kutengeneza nafasi na dakika ya 56, ikapata bao la utangulizi kupitia kwa Daizen Maeda akimalizia pasi nzuri ya nyota wa timu hiyo, Ritsu Doan.

Bao hilo la Japan, lilidumu kwa dakika sita tu, baada ya Anthony Elanga kuisawazishia Sweden dakika ya 62, akimalizia mpira wa Viktor Gyokeres na kurejesha upya matumaini ya timu hiyo katika mechi ya mwisho ya hatua ya makundi kusaka tiketi ya 32 bora.

Mabao hayo ya kipindi cha pili kwa kila timu, yakatosha kwa miamba hiyo ya soka kugawana pointi mojamoja na Uholanzi kuongoza kundi hilo la F na pointi saba, ikifuatiwa na Japan yenye tano, huku Sweden ikimaliza nafasi ya tatu na pointi nne, wakati Tunisia ndio iliyoburuza mkiani bila pointi zozote.

Japan inashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya nane tangu ilipoanza kushiriki kwa mara ya kwanza mwaka 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022 na 2026, huku mafanikio bora ni ya kuishia hatua ya 16, bora mara nne kuanzia 2002, 2010, 2018 na 2022.

Licha ubora wa Japan kutoka Bara la Asia ya Mashariki, ila taifa hilo bado limekuwa likiishia hatua ya 16, bora ya Kombe la Dunia kwa mara kadhaa, ikiwa ndio mafanikio yao makubwa kwenye michuano hiyo inayoendelea kujivunia katika rekodi ya kizazi hicho.

Kwa upande wa Sweden inashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya 13, tangu ilipoanza kushiriki kwa mara ya kwanza mwaka 1934, 1938, 1950, 1958, 1970, 1974, 1978, 1990, 1994, 2002, 2006, 2018 na 2026, ikiwa ni miongoni mwa timu zenye rekodi bora na za kuvutia kutokea Barani Ulaya.

Mafanikio makubwa kwa Sweden ni kufika hadi fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 1958, ikiwa ndio mwenyeji, ambapo kikosi hicho kilikosa ubingwa baada ya kuchapwa na Brazil mabao 5-2, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Rasunda, Juni 29, 1958.

Pia, Sweden ni miongoni mwa timu zilizomaliza mshindi wa tatu mara mbili ambapo ilianza mwaka 1950, katika fainali hizo zilizofanyika Brazil, kisha ikarudia tena mwaka 1994, kwenye michuano hiyo iliyofanyika Marekani kama ilivyokuwa kwa sasa.