Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta apata pigo, kumpoteza kamanda

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Kocha msaidizi wa Arteta, Carlos Cuesta anajiandaa kwenda kutajwa kuwa kocha mpya wa Parma akiwa na umri wa miaka 29.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta anaripotiwa kupata pigo baada ya kuripotiwa kwamba atampoteza mtu muhimu kwenye benchi lake la ufundi katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Kocha msaidizi wa Arteta, Carlos Cuesta anajiandaa kwenda kutajwa kuwa kocha mpya wa Parma akiwa na umri wa miaka 29.

Cuesta - ambaye alijiunga kwenye benchi la ufundi la Arsenal kumsaidia Arteta mwaka 2020 anajiandaa kwenda kutengeneza historia huko Serie A baada ya kupata fursa hiyo muhimu.

Mhispaniola huyo ataenda kuwa kocha mwenye umri mdogo zaidi huko Italia katika karne hii. Mzaliwa huyo wa Mallorca anatarajia kuichukua Parma akiwa na umri wa miaka 29, miezi 10 na siku 20.

Jambo hilo litamfanya Cuesta kuwa nyuma ya Elio Loschi, ambaye aliichukua kuinoa Triestina mwaka 1939 alipokuwa na umri wa miaka 29, miezi tisa na siku 20.

Kwa mujibu wa gwiji wa usajili, Fabrizio Romano, Arsenal ipo kwenye mazungumzo na Parma na jambo hilo lipo kwenye hatua ya mwisho. Na kinachoelezwa, mabosi wa Arsenal watafungua milango ya kocha Cuesta kuondoka. Hilo litakuwa pigo kwa Arteta, ambaye atapoteza msaidizi wake muhimu aliyemsaidia kuibadili Arsenal na kuwa timu ya kushindania mataji.

Cuesta alifanya kazi kwa mafanikio pia kwenye timu za Atletico Madrid na Juventus, alipokuwa kocha msaidizi kwenye vikosi vya timu za umri chini ya miaka 17. Na alitua Arsenal miezi tisa tangu Arteta alipochukua mikoba ya kuinoa timu hiyo kutoka kwa Unai Emery.