Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal kwa hiki kikosi hutoki!

Muktasari:

  • Msimu huu imekwama tena mbele ya Liverpool na msimu ujao bila shaka Man City itarudi na nguvu mpya, sambamba na miamba ya Anfield itakayotaka kutetea taji, jambo hilo litaifanya Arsenal kukabiliana na vita kali kwenye kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao.

LONDON, ENGLAND: BAADA ya kuchuana jino kwa jino na Manchester City kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England kwa misimu miwili mfululizo, Arsenal tatizo lao la kumaliza ukame wa mataji linazidi kuwa kubwa.

Msimu huu imekwama tena mbele ya Liverpool na msimu ujao bila shaka Man City itarudi na nguvu mpya, sambamba na miamba ya Anfield itakayotaka kutetea taji, jambo hilo litaifanya Arsenal kukabiliana na vita kali kwenye kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amekiri timu yake msimu huu haina ubora wa kutosha ukilinganisha na msimu uliopita. Kutokana na hilo, bila shaka Arsenal itaingia sokoni kukijenga upya kikosi chake ili kiwe na uwezo wa kuchuana na wababe wengine kwenye mbio za ubingwa.

1.Kipa na mabeki; Eneo moja ambalo Arsenal imekamilika vizuri ni beki. Arsenal imetengeneza safu ya ulinzi bora kabisa kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita na msimu huu.

Myles Lewis-Skelly ameibuka kwenye beki ya kushoto, wakati Riccardo Calafiori ameanza maisha kibabe katika nafasi hiyo licha ya majeraha kumharibia kiasi katika msimu wake huu wa kwanza kwenye EPL, huku Oleksandr Zinchenko akitarajiwa kuondoka.

Upande mwingine wa kulia kuna Jurrien Timber, Takehiro Tomiyasu na Ben White, ambao watakuwa na kazi ya kumlinda kipa David Raya, huku mabeki wa kati matata kabisa ni Gabriel na William Saliba, ambaye kocha Arteta anaamini atabaki kwenye kikosi na kuachana na ishu za Real Madrid. Yupo pia Jakub Kiwior ambaye ameonyesha kiwango bora tangu alipoumia Gabriel Magalhaes.

2.Viungo; Tangu dili lake la kwenda Liverpool kushindwa kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana, kiungo Martin Zubimendi amekuwa kwenye mjadala mzito. Arsenal inaonekana kuwa kwenye nafasi kubwa ya kumchukua staa huyo wa Real Sociedad ili kwenda kuboresha safu ya kiungo ya miamba hiyo ya Emirates sambamba na Martin Odegaard, Mikel Merino, Declan Rice na Thomas Partey kama atabaki kwenye kikosi hicho. Kiungo Jorginho ataondoka, lakini wasiwasi wa Zubimendi ni kwamba yupo pia kwenye mipango ya kocha mtarajiwa wa Real Madrid, Xabi Alonso.

3.Washambuliaji; Hili ni eneo lililokuwa tatizo kubwa kwenye kikosi cha Arsenal hasa kwenye nusu ya pili ya msimu huu kutokana na kuandamwa na majeruhi. Washambuliaji Kai Havertz, Gabriel Jesus na Bukayo Saka walipata majeraha na kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kitendo kilichomlazimisha Arteta kumtumia kiungo Merino kwenye eneo la mshambuliaji wa kati, huku Leandro Trossard (30) umri ukianza kumtupa mkono na Gabrielli Martinelli akitegemea mbio tu kuliko ubunifu. Kutokana na hilo, ndio maana Arsenal imelenga kufanya usajili wa mastraika wa viungo wa dunia kama Viktor Gyokeres, Benjamin Sesko na Alexander Isak, ikiamini straika yeyote atakayenaswa hapo atakwenda kuifanya Arsenal kuwa tishio kwenye fowadi yake kwa msimu ujao, akisimama katikati ya mawinga Bukayo Saka kulia, Havertz kushoto na Odegaard kwenye Namba 10. Hicho kikosi hutoki!