Arsenal inashusha kitasa huko

Saturday July 17 2021
arsenal pic

LONDON, ENGLAND. MMESIKIA? Arsenal ipo kwenye hatua nzuri ya kuipata saini ya beki kisiki wa  Brighton  na England  Ben White, 23, katika dirisha hili.
Taarifa zinadai mabosi wa Arsenal wamekuwa kwenye kikao kizito na mabosi wa Brighton ili kukamilisha dili la staa huyo ambaye timu yake imeripotiwa kuhitaji kiasi kisichopungua Pauni 50 milioni ili kumuuza.
Arsenal inamuangalia fundi huyo kama mbadala wa David Luiz ambaye ameachwa kwenye dirisha hili  baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye Ligi Kuu England kwa msimu uliopita ambapo alicheza mechi 39 za michuano yote.
Luiz ambaye amefikia uamuzi wa kutosaini mkataba mpya anahusishwa na  ofa ya kujiunga tena na PSG.

Advertisement