Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arbeloa alalamikia VAR, Madrid ikinyimwa penalti dhidi ya Girona

Muktasari:

  • Madrid ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Girona Ijumaa usiku, ambapo bao la kipindi cha pili la Federico Valverde lilisawazishwa na Thomas Lemar.

Kocha wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa amekosoa vikali uamuzi wa klabu yake kutopewa penalti baada ya Kylian Mbappe kuchezewa vibaya kwenye eneo la boksi katika mechi ya La liga dhidi ya Girona, akidai hadithi imekuwa ni ile ile tu na kila siku inatokea kwao.

Madrid ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Girona Ijumaa usiku, ambapo bao la kipindi cha pili la Federico Valverde lilisawazishwa na Thomas Lemar.

Mbappe aliingia ndani ya eneo la hatari la Girona akiwa na mpira, lakini akagongwa na mkono uliokuwa umeinuliwa na beki Vitor Reis.

Staa huyo alianguka ndani ya boksi, lakini malalamiko yake ya kupewa penalti yalipuuzwa na mwamuzi pamoja na VAR.

Aidha, alijeruhiwa usoni kiasi cha damu kumwagika hali iliyohitaji afanyiwe matibabu kwa muda kidogo ili kuwa sawa.

Baada ya mechi, Arbeloa alisema:"Ile ilikuwa ni penalti katika mechi inayocherzwa hapa duniani na hata mwezini.Sio mimi tu hata mtu mwingine yeyote hawezi kuelewa. Nashangaa kwanini VAR, haikuingilia, inaonekana inafanya kazi pale wao wanapotaka, na pale wasipotaka haifanyi hivyo. Ilikuwa faulo ya wazi. Tumekuwa na matatizo mengi na waamuzi. Hata kwenye mechi ya Mallorca, ni hadithi ile ile.”

Sare hiyo imepunguza zaidi matumaini ya Madrid kuwafikia wapinzani wao Barcelona katika mbio za ubingwa wa La Liga. Kwa sasa kikosi hicho chaa Arbeloa kipo nyuma kwa pointi tisa dhidi ya Barcelona.

Madrid kwa sasa inahamishia nguvu zao kwenda Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako wana mechi ya marudiano ya robo fainali dhidi ya Bayern Munich huko Ujerumani katika dimba la Allianz Arena. Madrid ina mlima mrefu wa kupanda kwani katika mechi ya mkondo wa kwanza ilipokea kichapo cha mabao 2-1.