Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Antony ataka kubakia Hispania

Muktasari:

  • Staa huyu wa kimataifa wa Brazil amezivutia timu nyingi barani Ulaya kutokana na kiwango alichoonyesha tangu alipotua Betis kwa mkopo baada ya kuanza msimu vibaya akiwa na Manchester United.

MADRID, HISPANIA: WINGA wa Manchester United ambaye msimu uliomalizika alikuwa akicheza kwa mkopo Real Betis, anadaiwa kutaka kuendelea kusalia nchini Hispania ambako Atletico Madrid inafanya kila linalowezekana ili kumnasa.

Staa huyu wa kimataifa wa Brazil amezivutia timu nyingi barani Ulaya kutokana na kiwango alichoonyesha tangu alipotua Betis kwa mkopo baada ya kuanza msimu vibaya akiwa na Manchester United.

Antony mwenye umri wa miaka 25, mkataba wake na Man United unatarajiwa kumalizoika mwaka 2027 kwa msimu huu akiwa na timu zote jumla amecheza mechi 36 za michuano yote na kufunga mabao tisa.

Baadhi ya malejendi wa zamani wa Betis wamekuwa wakiupigia sana kelele uongozi wa timu hiyo kwamba uhakikishe Antony anabaki huku baadhi wakiweka wazi kuwa wapo tayari hata kutoa  gari kwa ajili ya kumteka ikiwa itahitaji kufany hivyo ili abaki.

Hata hivyo, changamoto kubwa kwa timu hii inaonekana kuwa ni mshahara wake unaofikia Pauni 200,000 kwa wiki ambao ikiwa watahitaji abaki lazima waupunguze kwani hawatoweza kulipa kiasi chote hicho.

Hadi sasa, Antony hajatoa uamuzi wowote juu ya hatma yake licha kuelezwa kuwa timu nyingi zimeshaanza mazungumzo na wawakilishi wake.

Antony ambaye alisajiliwa chini ya Erik ten Hag mwaka 2022, akitokea Ajax alionekana kuwa na kipindi kigumu zaidi chini ya kocha Ruben Amorim  ambapo katika mahojiano yake ya hivi karibuni aliweka wazi kwamba alipoteza kabisa matumaini ya shauku ya kucheza mpira kutokana na nyakati zake akiwa na mashetani hao wekundu kwa sababu hakuwa anapata nafasi na alipopata hakuonyesha kiwango kilichotarajiwa.