Antonio Conte afunguka ishu ya McTominay
Muktasari:
- Staa huyo raia wa Scotland amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu licha ya kipigo hicho na uliopita alifunga mabao 12 akishinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu na alishinda namba 18 katika orodha ya washindi wa Ballon d’Or.
NAPLES, ITALIA: KOCHA wa Napoli, Antonio Conte, amesema hana shida kabisa na huduma ya kiungo wake, Scott McTominay kutokana na kile anachofanya uwanjani, huku akimweka kando kwenye orodha ya wachezaji ambao anaweza kuwabebesha lawama baada ya kipigo cha mabao 6-2 kutoka kwa PSV kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki iliyopita.
Conte amesema kuhusu McTominay: “Ni soka. Wakati mwingine unapaswa kukubali, lakini sina shida na kijana wangu.”
Staa huyo raia wa Scotland amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu licha ya kipigo hicho na uliopita alifunga mabao 12 akishinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu na alishinda namba 18 katika orodha ya washindi wa Ballon d’Or.
McTominay, 28, ameshafunga mabao matatu akitokea kwenye kiungo msimu huu, lakini Napoli sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, pointi mbili nyuma ya vinara AC Milan.
Uwepo wa tetesi za kuwa na changamoto kutoka kwa mashabiki kutokana na umaarufu wake inaelezwa huenda akaondoka na kurudi England.
Chanzo kilibainisha: “Scott alipenda baadhi ya vitu kwenye maisha ya Italia na ndio maana alitamba msimu uliopita. Kufurahiwa na mashabiki ni kitu kizuri, lakini hilo linampa wakati mzuri. Wanamchukulia kama mungu kwao na hilo linampa wakati mgumu anapokuwa mazoezini.”