Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ancelotti amfungulia mlango Neymar Kombe la Dunia 2026

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Neymar, ambaye kwa mara ya mwisho alichezea Seleção Oktoba 2023, alikuwa nje ya kikosi kilichocheza mechi za kirafiki mwezi Machi dhidi ya Ufaransa na Croatia.

BRASILIA, BRAZIL: Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Carlo Ancelotti amesema hajaondoa kabisa uwezekano wa kumjumuisha nyota Neymar Jr. katika kikosi kitakachoshiriki Kombe la Dunia 2026, endapo atathibitisha ubora na utimamu wa mwili wake.

Neymar, ambaye kwa mara ya mwisho alichezea Seleção Oktoba 2023, alikuwa nje ya kikosi kilichocheza mechi za kirafiki mwezi Machi dhidi ya Ufaransa na Croatia.

Hata hivyo, Ancelotti amesema bado mshambuliaji huyo yuko katika mchakato wa kuangaliwa na shirikisho la soka la Brazil (CBF) pamoja na benchi la ufundi.

Mchezaji huyo, 34 amewahi kushiriki Kombe la Dunia mara tatu (2014, 2018 na 2022), na ni mfungaji bora wa muda wote wa Brazil akiwa na mabao 79 katika mechi 128, akimpita Pelé.

Ancelotti alisema: “Kwa sasa anafanyiwa tathmini na CBF na mimi pia. Bado ana miezi miwili ya kuonyesha kama anaweza kucheza Kombe la Dunia. Nitawaita wachezaji walio fiti kimwili.”

Kocha huyo ameongeza baada ya Neymar kupata jeraha la goti mwezi Desemba, ameanza kurejea vizuri na hata kufunga mabao, jambo linaloonyesha maendeleo chanya.

“Neymar bado hayupo katika kiwango cha asilimia 100, ndiyo maana hakuwepo kwenye orodha ya awali. Lakini kama atafikia ubora wake wa kimwili, anaweza kuwa sehemu ya timu,” alisema Ancelotti.

Tangu arejee kucheza mwishoni mwa Februari, Neymar ameonyesha kiwango kizuri akiwa na mabao matatu na pasi mbili za mabao katika mechi nne, akionekana kurejea taratibu kwenye makali yake.

Hata hivyo, bado anapitia mpango maalum wa mazoezi na tiba ya kurejesha nguvu (PRP) ili kumuweka katika hali bora kuelekea mwisho wa mwaka.

Neymar mwenyewe amekiri kuwa bado anataka kucheza Kombe la Dunia, akisema anaamini anaweza kuisaidia Brazil licha ya kuwa katika hatua za mwisho za maisha yake ya kimichezo ya kimataifa.