Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amad Diallo amkubali Michael Carrick, asema freshi tu

DIALO Pict

Muktasari:

  • Safari hiyo ni sehemu ya kambi maalum ya mazoezi iliyoandaliwa na uongozi wa klabu, ili kuiweka timu katika hali nzuri katika kipindi hiki ambacho hawajacheza mechi ya kimashindano kwa muda mrefu.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Michael Carrick ameendelea kuungwa mkono na wachezaji wa timu hiyo ambao wameendela kusisitiza wanahitaji apewe mkataba wa kudumu.

Kocha huyo, 44, ambaye aliwahi kuwa kiungo wa Man United kabla ya kustaafu na kugeukia ukocha, amekuwa na kipindi kizuri cha muda mfupi tangu achukue mikoba kutoka kwa Ruben Amorim na Darren Fletcher  Januari mwaka huu.

Ameiongoza Man United kupata ushindi katika mechi saba, sare mbili na kupoteza mechi moja tu dhidi ya Newcastle United katika mechi 10 alizosimamia ambazo zote ni za Ligi Kuu England.

Kwa sasa Man United ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo, ikiwa kwenye mstari mzuri wa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Carrick alichaguliwa katika nafasi hiyo baada ya kumshinda aliyekuwa kocha wa zamani na gwiji wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer.

Katika mahojiano na waandishi wa habari, mastaa wa Man United Amad Diallo na Bryan Mbeumo walipoulizwa kuhusu kocha kuendelea kubakia, Diallo amesema: "Kwa kweli si jukumu letu sisi wachezaji kuamua mustakabali wake, lakini amekuwa mtu mzuri sana. Amefanya mengi kwa timu, ana uzoefu mkubwa, anaijua klabu vizuri, amekulia hapa. Tunaamini ndiye mtu sahihi na tunafurahia sana kile anachokifanya kwa sasa. Tumejifunza mengi chini yake. Sio sisi tunaoamua, lakini tutakuwa na furaha ikiwa atabaki."

Alipoulizwa kama wachezaji wenyewe huwa wanajadili suala la kocha kubaki, Diallo alijibu: “Kama nilivyosema, anaijua klabu, aliichezea, ana uzoefu mkubwa wa kuongoza. Hajakuwa hapa kwa muda mrefu lakini amefanya vizuri sana. Uhusiano wake na kila mchezaji ni mzuri na wakati mwingine unahitaji aina hii ya kocha ili kuirudisha klabu mahali inapostahili kuwa. Kwa maoni yangu binafsi, ndiye mtu sahihi, lakini sisi  wachezaji sio tunaoamua."

Man United imesafiri kwenda Dublin, Ireland kwa kambi ya siku tatu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wao wa Jumatatu dhidi ya Leeds United kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Safari hiyo ni sehemu ya kambi maalum ya mazoezi iliyoandaliwa na uongozi wa klabu, ili kuiweka timu katika hali nzuri katika kipindi hiki ambacho hawajacheza mechi ya kimashindano kwa muda mrefu.