Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amad atupia Ivory Coast ikishinda kidude

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha Tembo kikiwa na dhamira ya kuwa timu ya kwanza kutetea taji la Afcon tangu ilipofanya hivyo Misri 2010 ilipoteza nafasi nyingi za kufunga kwenye kipindi cha kwanza dhidi ya timu hiyo inayoshika nafasi ya 102 kwenye viwango vya ubora vya Fifa.

MARRAKECH, MOROCCO: STAA wa Manchester United, Amad Diallo amefunga bao maridadi kuipa mabingwa watetezi wa Afcon, Ivory Coast ushindi muhimu dhidi ya Msumbiji kwenye mechi yao ya kwanza ya Kundi F kwenye mashindano ya Afcon 2025 iliyofanyika Marrakech.

Kikosi hicho cha Tembo kikiwa na dhamira ya kuwa timu ya kwanza kutetea taji la Afcon tangu ilipofanya hivyo Misri 2010 ilipoteza nafasi nyingi za kufunga kwenye kipindi cha kwanza dhidi ya timu hiyo inayoshika nafasi ya 102 kwenye viwango vya ubora vya Fifa.

Amad alifunga bao pekee lililokipa ahueni kikosi cha kocha Emerse Fae alipoafanya ubao wa matokeo usomeke 1-0 dakika ya nne baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, alipomalizia kazi nzuri ya kiungo Franck Kessie, akifunga kwa mpira wa chini uliopita kwenye uvungu wa miguu ya beki wa Msumbiji, anayekipiga Sunderland, Reinildo.

Kipa wa Msumbiji, Ernan alikuwa bize sana kwenye kipindi cha kwanza, alipookoa mpira wa ticktack ya Yan Diomande na kumgomea Kessie alipopiga kichwa akiwa karibu na goli.

Ghislain Konan alikaribia kabisa kufunga wakati Amad alipowahadaa mabeki wa Msumbiji kwa kuingia ndani akitokea upande wa kushoto. Katika mechi hiyo, Ivory Coast ilipoteza nafasi nyingi za kufunga, huku kipa wa Msumbiji Ernan akifanya kazi ya ziada.

Lakini, ushindi huo ni muhimu kwa Ivory Coast katika mpango wao wa kutetea taji hilo la ubingwa wa Afrika, AFCON.