Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alonso ajiingiza kesi ya Barca

Muktasari:

  • Soka la Hispania kwa zaidi ya miaka miwili na nusu limegubikwa na kesi inayofahamika kama 'The Negreira case' na kwamba uchunguzi wake unaendelea kufanyika.

MADRID, HISPANIA: KOCHA wa Real Madrid, Xabi Alonso amemtaka rais wa miamba hiyo Florentino Perez kutafuta haki baada ya kuwapo na kashfa ya rushwa inayowahusisha mahasimu wao wakuu kwenye La Liga, Barcelona.

Soka la Hispania kwa zaidi ya miaka miwili na nusu limegubikwa na kesi inayofahamika kama 'The Negreira case' na kwamba uchunguzi wake unaendelea kufanyika.

Barca iliwahi kukiri kufanya malipo ya Euro 8.4 milioni katika kampuni inayohusishwa kuwa na uhusiano na aliyekuwa bosi wa waamuzi wa soka Hispania, Jose Maria Enriquez Negreira kati ya mwaka 2001 na 2018. Lakini, rais wa Barcelona, Joan Laporta alifafanua malipo hayo yalifanywa kwa ajili ya kuwezesha kufanya skauti ya waamuzi wa La Liga.

Negreira, kwa upande wake alikana kupewa rushwa ili awashawishi waamuzi. Hata hivyo, majibu yake hayaonekani kumtosheleza rais wa Real Madrid, Perez ambaye amelitaja tukio hilo kuwa ni kashfa kubwa kwenye historia ya soka wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wiki hii katika kuelekea Krismasi.

"Ni kitu kinachoshangaza kuona hii kitu imeachiwa Real Madrid ipambane peke yake," alisema Perez.

"Hivi inawezekana vipi raisi wa waamuzi anatutaka tusahau juu ya jambo hilo? Tunawezaje kusahau kashfa kubwa kabisa katika historia ya soka? Inakuwaje shirikisho la soka la Hispania na La Liga linafanya hivi? Wajibu wao ni kuhakikisha uadilifu."

Perez aliongeza: "Inawezekana kuna baadhi ya klabu zilishuka daraja kutokana na tukio hili. Soka letu limeharibika, hivyo haki inapaswa kufanyika."

Barcelona kwa sasa inaongoza msimamo wa La Liga kwa tofauti ya pointi nne, licha ya Real Madrid kuwahi kuongoza kwa tofauti ya pointi tano mwishoni mwa Oktoba.