Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alexander-Walker aanza mambo, abeba tuzo ya kwanza NBA 2026

Muktasari:

  • Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka kwa mchezaji aliyeonyesha mabadiliko makubwa zaidi ya kiwango chake uwanjani, Alexander-Walker aliwabwaga Deni Avdija na Jalen Duren, hivyo kuifanya Hawks kuwa miongoni mwa timu chache zinazozalisha wachezaji bora walioboreshwa.

ATLANTA, MAREKANI: NYOTA wa Atlanta Hawks, Nickeil Alexander-Walker, ameandika historia mpya baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji aliyeboreshwa zaidi (Most Improved Player – MIP) katika msimu wa NBA 2025–26.

Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka kwa mchezaji aliyeonyesha mabadiliko makubwa zaidi ya kiwango chake uwanjani, Alexander-Walker aliwabwaga Deni Avdija na Jalen Duren, hivyo kuifanya Hawks kuwa miongoni mwa timu chache zinazozalisha wachezaji bora walioboreshwa.

Ushindi huu unakuja mwaka mmoja baada ya Dyson Daniels kushinda tuzo hiyo, jambo linaloonyesha wazi mafanikio ya mfumo wa maendeleo wa klabu hiyo.


MABADILIKO YAKE

Katika msimu huu, Alexander-Walker ameonyesha kiwango cha kipekee ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika maisha yake ya kikapu. Amefunga wastani wa pointi 20.8 kwa kila mchezo, ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya wastani wake katika misimu sita ya awali. Hii ni ishara tosha ya mabadiliko yake makubwa  kutoka mchezaji wa kawaida hadi kuwa tegemeo muhimu ndani ya kikosi.

Mbali na ufungaji, pia alionyesha kiwango kikubwa katika vipengele vingine vya mchezo. Alimaliza msimu akiwa na wastani wa pasi za mwisho 3.7, rebound 3.4 na kuiba mipira 1.3 kwa kila mchezo.

Ufanisi wake wa mitupio ulikuwa wa kiwango cha juu, akitupia kwa asilimia 46 ya mitupio ya kawaida, asilimia 40 ya alama tatu na asilimia 90 ya mitupio ya adhabu.

MUDA WA KUCHEZA

Mabadiliko yake hayakutokea kwa bahati mbaya. Alexander-Walker alipata nafasi kubwa zaidi ya kuonyesha uwezo wake baada ya kuongezewa muda wa kucheza. Katika msimu huu, alicheza jumla ya dakika 2,603 ongezeko kubwa ukilinganisha na misimu iliyopita.

Kuongezeka kwa muda huo kulimruhusu kujenga kujiamini, kuimarisha mbinu zake na kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Hawks. Alifunga idadi kubwa ya mipira ya alama tatu pamoja na mitupio ya adhabu, hali iliyoongeza mchango wake kwa timu kwa kiwango kikubwa.


NAFASI YAKE

Mwanzoni mwa msimu, Alexander-Walker alikuwa akitumika zaidi kama mchezaji wa akiba (sixth man). Hata hivyo, mambo yalibadilika haraka baada ya kuumia kwa nyota wa timu Trae Young na baadaye kuondoka kwake katika usajili wa kati ya msimu.

Katika dili hilo, Hawks walimpata CJ McCollum, lakini bado Alexander-Walker ndiye aliyeshika nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza.


MFUMO WA KUKUZA VIPAJI

Mafanikio haya yameibua tena sifa kwa mfumo wa kukuza vipaji wa Hawks chini ya kocha Quin Snyder. Timu hiyo imeonyesha uwezo mkubwa wa kuwapa nafasi wachezaji vijana na kuwasaidia kukua kwa haraka ndani ya mfumo unaowapa uhuru wa kucheza na kujiamini.

Wachezaji wengi wamefaidika na mfumo huo na ushindi wa tuzo ya MIP kwa miaka miwili mfululizo ni uthibitisho kwamba Hawks si tu timu ya ushindani, bali pia ni kituo muhimu cha maendeleo ya vipaji katika NBA.

FAMILIA YA KIKAPU

Alexander-Walker anatoka katika familia yenye historia ya mafanikio katika mpira wa kikapu. Binamu yake, Shai Gilgeous-Alexander wa Oklahoma City Thunder, ni mmoja wa nyota wakubwa wa NBA na mshindi wa tuzo ya MVP msimu uliopita.

Uhusiano huu unaongeza uzito wa mafanikio yake, ukionyesha kuwa mafanikio hayo si ya bahati bali ni matokeo ya mazingira ya ushindani na vipaji vilivyokuzwa kwa muda mrefu.


TUZO NYINGINE NBA

Mbali na tuzo ya MIP, NBA imeshatangaza baadhi ya washindi wengine wa tuzo za msimu huu. Victor Wembanyama ametwaa tuzo ya mlinzi bora wa mwaka huku Keldon Johnson akishinda tuzo ya mchezaji bora wa akiba.

Aidha, macho na masikio ya mashabiki sasa yanaelekezwa kwenye tuzo kubwa zaidi ya MVP, ambapo majina kama Nikola Jokic na Shai Gilgeous-Alexander yanatajwa.