Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Al Hilal inabalaa yabeba tena ugenini

Muktasari:

  • Al Hilal ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 70 ikicheza mechi 30 ikifuatiwa na APR yenye pointi 59 ikibakiza mechi tatu ambapo hata ikishinda mechi zote zilizobaki haitaweza kukaa nafasi ya kwanza.

AL Hilal imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Rwanda ikiwa imebakiza mechi nne kumaliza msimu wa 2025-2026.

Al Hilal ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 70 ikicheza mechi 30 ikifuatiwa na APR yenye pointi 59 ikibakiza mechi tatu ambapo hata ikishinda mechi zote zilizobaki haitaweza kukaa nafasi ya kwanza.

Huu ni msimu wa kwanza kwa Al Hilal kushiriki ligi hiyo ambapo msimu uliopita ilishiriki Ligi ya Mauritania na kuchukua ubingwa.

Al Hilal na Al Merrikh za Sudan zinashiriki Ligi ya Rwanda kwasababu ya hali hafifu za kiusalama zinazoendelea nchini kwao.

Al Merrikh kwa sasa ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 58 ikicheza mechi 30, nayo ikibakiza mechi nne kumaliza ligi.

Msimu huu wa 2025/26 Al Hilal ilishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) na ikaishia hatua ya robo fainali baada ya kutolewa na RS Berkane, Al Merrikh ikiishia hatua ya makundi Kombe la Shirikikisho Afrika (CAFCC)