34 zatangulia Kombe la Dunia 2026
Muktasari:
- Fainali za Kombe la Dunia 2026 zimepangwa kuanza Juni 11, 2026 na mechi ya ufunguzi itachezwa Estadio Azteca, Mexico City.
Nchi 34 zimejihakikishia kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazounguruma nchini Mexico, Marekani na Canada, baada ya kukamilisha mchakato wa kufuzu.
Fainali za Kombe la Dunia 2026 zimepangwa kuanza Juni 11, 2026 na mechi ya ufunguzi itachezwa Estadio Azteca, Mexico City.
Jana Jumatatu usiku Novemba 17, 2025, Ujerumani na Uholanzi ziliungana na timu nyingine 32 ambazo zilishafuzu kucheza fainali hizo, zikitokea barani Ulaya. Ujerumani ilipata nafasi hiyo baada ya ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Slovakia, mechi ikichezwa Red Bull Arena huku Uholanzi ikiichapa Lithuania 4-0.
Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitashirikisha mataifa 48, ikiwa ni ongezeko la timu 16. Kuanzia mwaka 1998 katika fainali zilziofanyika nchini Ufaransa, mataifa 32 yalikuwa yanashiriki na mara ya mwisho idadi hiyo ilionekana nchini Qatar mwaka 2022.
Hapa chini ni orodha kamili ya kila nchi iliyofuzu Kombe la Dunia 2026:
Wenyeji: Canada, Mexico, Marekani
Asia: Australia, Iran, Japan, Jordan, Qatar, Saudi Arabia, Korea Kusini, Uzbekistan
Afrika: Algeria, Cape Verde, Misri, Ghana, Ivory Coast, Morocco, Senegal, Afrika Kusini, Tunisia
Ulaya: Croatia, England, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, Norway, Ureno
Oceania: New Zealand
Amerika Kusini: Argentina, Brazil, Colombia, Ecuador, Paraguay, Uruguay