Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

17 waonyeshwa kadi nyekundu mechi moja

KADI NYEKUNDU Pict

Muktasari:

  • Viurugu hizo ambazo zilihusisha wachezaji wa pande zote mbili na wafanyakazi wengine wa timu hizo, zilitokea katika mechi ya mkondo wa pili ya robo fainali ya Kombe la Bolivia na ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

SUCRE, BOLVIA: MECHI moja ya soka Bolivia, Bara la Amerika Kusini ilishuhudiwa wachezaji 17 wakitolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na vurugu zilizoibuka kati ya timu za Blooming na Real Oruro.

Viurugu hizo ambazo zilihusisha wachezaji wa pande zote mbili na wafanyakazi wengine wa timu hizo, zilitokea katika mechi ya mkondo wa pili ya robo fainali ya Kombe la Bolivia na ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Sare hiyo ilisababisha Blooming kufuzu nusu fainali baada ya mechi ya kwanza kumalizika ikishinda 2-1 na baada ya mechi hiyo kumalizika, vurugu kubwa zilizuka.

Katika kipande cha video kilichosambaa mitandaoni kilionyesha wachezaji kutoka pande zote mbili wakiwa wanakabiliana kwa kupigana ngumi na kurushiana vitu na Polisi waliokuwa uwanjani walilazimika kutumia gesi ya machozi kudhibiti vurugu hizo.

Kwa mujibu wa gazeti la Bolivia, El Potosi, vurugu zilianza baada ya nyota wa Oruro, Sebastian Zeballos, kushikwa na wachezaji wa Blooming, kabla ya kujitoa na kuanza kurushiana nao ngumi.

Mchezaji mwenzake naye akaingilia ugomvi huo na kuanza kurusha ngumi ambazo zilizalisha rasmi vurugu hizo.

Kocha wa Oruro, Marcelo Robledo, kwa upande wake, alionekana akivaana na mmoja wa wafanyakazi wa benchi la ufundi la Blooming.

Zaidi ya polisi 20 waliokuwa na silaha na mbwa waliingia kiwanjani kwa ajili ya kutuliza ghaasia hizo.

Kocha wa Blooming, Mauricio Soria, baadae aliwaamuru wachezaji wake kwenda chumba cha kubadilisha nguo ili kuwatuliza.

Ripoti zinasema Oruro walikasirishwa baada ya kushindwa kufuzu nusu fainali, licha ya kuhitaji bao moja tu la kusawazisha.

Ripoti ya mchezo inaonyesha wachezaji saba wa Blooming na wanne wa Oruro walionyeshwa kadi nyekundu na refa Renan Castillo.

Vilevile baadhi ya maofisa wa benchi la ufundi wa timu zote  walionyeshwa kadi nyekundu.