Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mykhailo Mudryk aibuka na muonekano mpya akiwa kwenye adhabu

Muktasari:

  • Mchezaji huyo anafanya mazoezi peke yake baada ya kusimamishwa na Chama cha Soka England (FA).

LONDON,  ENGLAND: WINGA wa Chelsea, Mykhailo Mudryk ameonekana tofauti na alivyozoeleka, huku nyota huyo akiendelea na mazoezi binafsi wakati akiwa amefungiwa kujihusisha na soka.

Mchezaji huyo anafanya mazoezi peke yake baada ya kusimamishwa na Chama cha Soka England (FA).

Mudryk alipewa adhabu ya kusimamishwa kwa muda Desemba 2024 baada ya sampuli yake ya mkojo kubainika kuwa na dawa iliyopigwa marufuku michezoni ya meldonium, ambapo adhabu hiyo inamzuia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kufanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Chelsea au kutumia miundombinu ya klabu hiyo.

Kutokana na hali hiyo, amekuwa akikodisha uwanja wa klabu ya daraja la chini ya Uxbridge FC kwa ajili ya mazoezi.

Klabu hiyo inayoshiriki Southern League Premier Division South ipo takriban saa moja kutoka kituo cha mazoezi cha Cobham cha Chelsea. Mudryk pia ameajiri kipa pamoja na kocha binafsi ili kumsaidia kujiweka fiti wakati huu ambao yupo nje ya Ligi Kuu England.

Katika chapisho lake la hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii akiwa kwenye uwanja wa 3G wa Uxbridge, Mudryk alionyesha mwonekano mpya wa kushangaza.

Baada ya kujiunga na Chelsea Januari 2023 akiwa na nywele za rangi ya dhahabu zilizolazwa kwa nyuma, baadaye alizikata kuwa fupi kabla ya kusimamishwa. Hata hivyo, kwenye picha yake ya hivi karibuni ya Instagram, ameonekana akiwa na nywele ndefu zaidi za rangi ya kahawia hafifu pamoja na ndevu tofauti na alivyoonekana akiwa amenyoa kabisa mara ya mwisho alipocheza.

Mechi yake ya mwisho ilikuwa Novemba 28, 2024 dhidi ya Heidenheim katika Europa Conference League. Pia alikaa benchi dhidi ya Aston Villa siku tatu baadaye.