Lewandowski mkakati ni kutua Real Madrid tu sasa

Friday December 03 2021
Lewa PIC

TAYARI vigogo wa Real Madrid wameanza harakati za kuiwania saini ya straika wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Poland, Robert Lewandowski, 33, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo staa huyo amewasilisha barua ya kuomba kuondoka Munich ili kutafuta changamoto mpya.

Lewandowski ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Munich msimu huu amecheza mechi 20 za michuano yote na kufunga mabao 25.

Madrid inataka kumsajili Lewandowski kwa sababu ina asilimia nyingi za kuachana na winga wao Gareth Bale katika dirisha lijalo.

Lewandowski ni miongoni mwa wachezaji waliotarajiwa kushinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu lakini ilishindikana tuzo hiyo ikienda kwa supastaa wa PSG, Lionel Messi aliyeibeba kwa mara ya saba ikiwa ni rekodi ya dunia.

Mkataba wake Lewandowski unamalizika mwaka 2023.

Advertisement