Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiwango cha Garnacho chamkosha Fernandes

Fernandez Pict

Muktasari:

  • Man United ilitinga raundi ya nne ya michuano hiyo Jumapili iliyopita baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti 5-3 kufuatia sare ya bao 1-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Emirates. Fernandes alifunga bao la Man United baada ya pasi matata kabisa ya Garnacho.

MANCHESTER, ENGLAND: KIUNGO wa Manchester United, Bruno Fernandes amemmwagia sifa kinda wa miamba hiyo, Alejandro Garnacho baada ya kuonyesha kiwango bora wakati walipocheza pungufu uwanjani na kuichapa Arsenal kwenye Kombe la FA.

Man United ilitinga raundi ya nne ya michuano hiyo Jumapili iliyopita baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti 5-3 kufuatia sare ya bao 1-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Emirates. Fernandes alifunga bao la Man United baada ya pasi matata kabisa ya Garnacho.

Diogo Dalot alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa njano mbili kabla ya Gabriel Magalhaes kuisawazishia Arsenal muda mfupi baadaye. Kisha Arsenal ilipata penalti ya utata ambayo Martin Odegaard alikosa baada ya kipa Altay Bayindir kuipangua kabla ya kuudaka kabisa mpira.

Kipa huyo Mturuki alifanya kazi ya ziada kuokoa hatari kadhaa hadi mechi hiyo kufikia kwenye hatua ya kupigiana mikwaju ya penalti ambapo Bayindir, aliokoa mkwaju mmoja wa Kai Havertz na hivyo kufanya timu yake kutinga hatua inayofuata.

Licha ya kiwango bora cha kipa, Fernandes alihakikisha kwamba Garnacho anastahili sifa zake. Baada ya pasi ya Garnacho, Fernandes alipotumbukiza mpira kwenye nyavu alichokifanya kwenye kushangilia ni kuonyesha kidole kwa kinda huyo wa Kiargentina kwamba ndiye aliyestahili pongezi kubwa kwa bao hilo. Hiyo si mara ya kwanza kwa Fernandes kumsifu mshambuliaji huyo baada ya hivi karibuni kuonekana kukosa furaha, wakati alipofunga bao dhidi ya Leicester City na kisha hakushangilia.

 Lakini, Fernandes alimhamasisha mshambuliaji huyo kufurahia mpira na anapofunga bao, anapaswa kushangilia.

Garnacho amecheza mechi 29 za kwenye kikosi cha Man United msimu huu, akifunga mabao manane na asisti nne. Mkataba wake utaisha mwaka 2028.