Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

 England yachukua Euro kibabe ikilipa kisasi kwa Hispania

Basel, Uswis. Timu ya taifa ya wanawake ya England ‘Lionesses’ imeandika historia mpya kwa kutwaa taji la Ulaya kwa Wanawake 2025 baada ya kuilaza Hispania kwa penalti 4-2 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye dimba la St. Jakob-Park.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 katika dakika 120 na kulazimisha mshindi kupatikana kwa njia ya mikwaju ya penalti.

England imefanikiwa kulipa kisasi cha kufungwa na Hispania katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2023 kwa bao 1-0.

Bao la kwanza la mchezo huo lilifungwa na Hispania katika dakika ya 38 kupitia nyota wake Aitana Bonmatí, kabla ya England kusawazisha kipindi cha pili katika dakika ya 57 kupitia kwa Alessia Russo aliyeunganisha krosi ya Chloe Kelly.

Penalti za England zimefungwa na Chloe Kelly, Georgia Stanway, Lauren Hemp, na Keira Walsh, huku kipa wao Hannah Hampton akiokoa penalti mbili.

Kwa ushindi huo, England wamefanikiwa kutwaa taji la pili la Ulaya katika historia yao na la pili mfululizo baada ya lile la mwaka 2022, wakiendelea kuonesha ubabe katika soka la wanawake barani Ulaya.

Kocha wa England, Sarina Wiegman, aliwapongeza wachezaji wake kwa moyo wa kupambana na kusema ushindi huo ni wa kihistoria kwa taifa hilo.

Wachezaji Mariona Caldentey, Aitana Bonmatí na Salma Paralluelo walilififisha matumaini ya Hispania baada ya kupoteza mikwaju ya penalti.