Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Donnarumma mbioni kusepa, PSG yasaka mtu

TETESI Pict

Muktasari:

  • Vigogo hawa wanahitaji sana huduma ya Donnarumma kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu atue katika kikosi cha PSG.

INAELEZWA Manchester United na Manchester City zote zinavutiwa na kipa wa Paris St-Germain na timu ya taifa ya Italia, Gianluigi Donnarumma, mwenye umri wa miaka 26.

Vigogo hawa wanahitaji sana huduma ya Donnarumma kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu atue katika kikosi cha PSG.

Mabosi wa PSG wapo tayari kumuuza kipa huyu wa kimataifa wa Italia na tayari imeshaanza kuangalia mbadala wake ambapo inamlenga kipa wa Lille na timu ya taifa ya Ufaransa, Lucas Chevalier mwenye umri wa miaka 23.

Kipa huyu namba mbili wa timu ya taifa ya Ufaransa anaripotiwa kuwa ameshafanya hadi makubaliano binafsi na mabosi wa PSG na atasaini mkataba wa miaka mitano.

Kwa upande wa Lille nayo ipo tayari kumwachia kwa Euro 40 milioni jambo ambalo linazidi kutoa ishara ya kwamba Donnaruma ataondoka.

Timu nyingi zimezidi kumiminika kutaka kumsajili Donnarumma kwa sababu mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu ujao lakini hadi sasa bado hajakubali kusaini mkataba mpya.

Msimu uliopita Donnaruma mwenye umri wa miaka 26, aliisaidia PSG kushinda mataji matatu kwa pamoja ikiwemo Ligi ya Mabingwa ameripotiwa kukataa ofa ya mkataba mpya aliyowekewa mezani hadi sasa.

Galatasaray pia wanatarajia kufanya mazungumzo kuhusu Donnarumma, ambaye yuko karibu kuingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake huko Paris.


William Saliba

REAL Madrid iko tayari kusubiri hadi mwakani kabla ya kuwasilisha ofa kwenda Arsenal ili kumsajili beki kisiki wa The Gunners na timu ya taifa ya Ufaransa, William Saliba, mwenye umri wa miaka 24.

Saliba ambaye mkataba wake na Arsenal unamalizika mwaka 2027, amekuwa akitajwa kuwa katika rada za Madrid kwa muda mrefu lakini ameonyesha kuwa na mpango wa kubakia Arsenal. Msimu uliopita, Saliba  alicheza mechi 51 za michuano yote.


Francesco Pio Esposito

MANCHESTER United inafikiria kuwasilisha ofa mpya kwenda Inter Milan kwa ajili ya kuipata  saini ya mshambuliaji wa klabu hiyo na Italia, Francesco Pio Esposito, mwenye umri wa  miaka 20, katika dirisha hili.

Awali, Man United iliwasilisha ofa ya kwanza lakini vigogo wa Inter waliikataa kwa sababu hawako tayari kumruhusu fundi huyu aondoke lakini wanaweza kufikia uamuzi huo ikiwa itapokea ofa nono.


Kenan Yildiz

CHELSEA inataka kuwasilisha ofa mpya ya Pauni 65 milioni kwenda Juventus kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo na Uturuki, Kenan Yildiz, baada ya ofa yao ya kwanza ya Pauni 60 milioni kukataliwa.

Juventus inataka takribani Pauni 70 milioni ili kumuuza fundi huyu mwenye umri wa miaka 20. Ikiwa pesa hiyo haitatolewa, Juventus imesisitiza kuwa Kenan ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2029, hatouzwa.

Kenan alifanya vizuri katika michuano ya Kombe la Dunia kwa klabu msimu uliopita ambapo katika mechi nne alifunga mabao matatu.


Antony

AL Nassr na Al-Hilal ndio timu mbili kutoka Saudi Arabia zinazohitaji kumsajili mshambuliaji wa Manchester United ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Real Betis, Antony, 25.

Awali, Betis ilikuwa ikipambana kuhakikisha anarudi katika kikosi chao kutokana na kiwango bora alichoonyesha lakini inaonekana kuwa ngumu kutokana na mshahara ambao anauhitaji.


Roberto Piccoli

WEST Ham na Benfica zinapanga kutoa ofa kwenda  Cagliari kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo na Italia, Roberto Piccoli mwenye umri wa miaka 24, katika dirisha hili. Mabosi wa Cagliari wapo tayari kumuuza staa huyu na inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 26 milioni kama ada yake ya uhamisho. Mkataba wa Piccoli unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Igor Paixao

LEEDS ipo tayari kulipa Pauni 28 milioni kwenda Feyenoord kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo, Igor Paixao mwenye umri wa miaka 26, lakini inakumbana na ushindani mkali kutoka  kwa Marseille na Roma ambazo pia zinahitaji huduma ya fundi huyu wa kimataifa wa Brazil. Igor mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Jens Cajuste

BURNLEY imetuma wawakilishi wake kwenda Italia kwa ajili ya kuanza mazungumzo na Napoli juu ya kuipata huduma ya kiungo wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Sweden, Jens Cajuste mwenye umri wa miaka 25,  katika dirisha hili. Benchi la ufundi la Burnley limevutiwa sana na kiwango ambacho staa huyu alikionyesha msimu uliopita alipokuwa kwa mkopo Ipswich Town.